Na Lydia Lugakila - Misalaba Media,MBEYA
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Jumanne Abdallah Sagini, ameitaka Kamati ya Maafa kuendelea kutoa misaada ya chakula na vifaa muhimu vya kibinadamu kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea Novemba 3, 2026, katika eneo la Nzovwe jijini Mbeya.
Akizungumza Novemba 4, 2026, wakati wa ziara ya kutembelea waathirika hao, Sagini amesema Serikali ipo pamoja nao na itahakikisha inawasaidia kukabiliana na hali ngumu wanayoipitia baada ya kupoteza makazi, chakula na mali zao kutokana na mafuriko hayo.
Amesema Serikali itasimama nao bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu, huku akieleza kuwa ziara hiyo imebeba pia salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha ili kuepuka madhara zaidi, akisisitiza umuhimu wa kuzingatia usalama wao na familia zao.
"Nadhani kila mmoja ameweza kushuhudia madhara makubwa yaliyotokea hizi ni mvua ndogo tu zimenyesha ndani ya nusu saa, lakini madhara yake ni makubwa mno.
nilazima tuwe makini na kuchukua tahadhari mapema ili kuepuka maafa zaidi," amesema Sagini.
Akielezea madhara ya mafuriko hayo, mmoja wa waathirika, Samson Bakari, amesema maji yaliingia kwa kasi na kusomba vyakula, nguo pamoja na samani mbalimbali za ndani ya nyumba.
"Maji yaliingia kwa kasi sana na kusomba vyakula, nguo na samani zote za ndani nyumba zetu zimejaa tope na familia nyingi hapa Nzovwe hatuna mahali pa kulala wala chakula cha kuwapa watoto," amesema Bakari.
Kwa upande wake, Josephat Mwanjesa amemshukuru Mkuu wa Mkoa pamoja na ujumbe wake kwa kufika mapema kuwafariji waathirika na kuwapatia matumaini ya kupata msaada kutoka serikalini.
"Tunashukuru sana Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kwa kujiunga nasi siku hii ya leo na kutuletea salamu za Rais Samia Kuwepo kwako hapa na ahadi ya misaada kumetupa matumaini mapya kwamba hatujatelekezwa kwenye janga hili," amesema Mwanjesa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamati ya Maafa, mvua iliyonyesha kwa muda usiozidi dakika 30 imesababisha uharibifu wa nyumba 21 na kuathiri kaya zisizopungua 43.
Ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa iliambatana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, viongozi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na wawakilishi wa Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross).
PROFESSOR MGOKO EP 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment