Na.Mwandishi wetu MWANZA: Shule ya Awali na Msingi ya Santa Edwin iliyopo Majengo Mapya, Nyegezi, Jijini Mwanza, imeendelea kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (Darasa la Saba) baada ya kupata wastani wa Daraja A katika matokeo yaliyotangazwa leo na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).Mafanikio hayo yanaonesha mwendelezo wa ufaulu mzuri wa wanafunzi wanaohitimu katika shule hiyo, ambayo imeendelea kuweka msisitizo katika utoaji wa elimu bora na malezi kwa watoto.Akizungumza kuhusu matokeo hayo.Mkurugenzi wa shule hiyo, Bwana Edwin Soko, amesema uongozi wa Santa Edwin utaendelea kuimarisha ubora wa elimu ili kuhakikisha wanafunzi wanapata maarifa na ujuzi unaoendana na mahitaji ya sasa.Soko amesema shule hiyo imejipanga kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na kuhakikisha inakuwa kinara wa ufaulu kila mwaka.Ameongeza kuwa maandalizi ya mwaka wa masomo kwa Mwaka 2027 yameanza, huku shule ikiendelea kupokea wanafunzi wapya na wanaohamia kutoka shule nyingine kwa madarasa yote.Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Santa Edwin, Bwana Hassan Ibrahimu, amesema anamshukuru Mungu kwa matokeo mazuri ya Daraja A yaliyoiwezesha shule hiyo kuwa miongoni mwa shule zinazofanya vizuri katika Mkoa wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla.Hassan amesema shule imeweka mikakati mbalimbali kwa mwaka 2027 ili kuendeleza na kuboresha zaidi ufaulu wa wanafunzi.“Mikakati yetu kwa mwaka 2027 ni kuendeleza ufundishaji bora kwa wanafunzi ili kupata matokeo bora zaidi, kuhakikisha wanafunzi wote wa madarasa ya mitihani wanaishi hapa shuleni ili walimu wapate muda wa kutosha katika maandalizi ya mitihani yao, pamoja na kuimarisha malezi na huduma bora kwa watoto wetu,” alisema Hassan.Pia amesema mikakati hiyo inalenga kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira mazuri ya kujifunzia, muda wa kutosha wa maandalizi ya mitihani na huduma zinazowawezesha kufikia malengo yao kitaaluma.Hassan ametoa wito kwa wazazi na walezi ambao bado hawajachagua Santa Edwin Pre and Primary School kuwaandikisha watoto wao katika shule hiyo ili wapate elimu bora.Aidha, amewashukuru wazazi ambao tayari wameichagua shule hiyo na kuwataka kuendelea kuwaamini zaidi, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya shule na wazazi katika kuhakikisha maendeleo ya watoto.Amesisitiza kuwa wazazi wanapaswa kulipa ada kwa wakati ili kuiwezesha shule kuendesha shughuli zake kwa ufanisi na kuendelea kutoa huduma bora za elimu.Santa Edwin Pre and Primary School ipo Majengo Mapya, Nyegezi, Jijini Mwanza, na inaendelea kupokea wanafunzi wanaohamia kwa madarasa yote kwa mwaka wa masomo 2027.Kwa mawasiliano na kujiunga na shule:07863498130768247274
PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment