Ajali hiyo ilitokea jana Februari 4, 2023 wakati wanasafirisha mwili kwenda kuzikwa mkoani Kilimanjaro ambapo 18 walifariki papo hapo.
Wawili hao wamefariki mmoja akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Bombo na mwingine Muhimbili.
Taarifa ya kuongezeka idadi ya marehemu hao imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba kwenye ibada ya kuaga miili hiyo inayofanyika Hospitali ya Magunga wilayani Korogwe.
"Tutavunja itifaki kidogo kutokana na kuongezeka idadi ya waliofariki, itabidi tukiendelea na ibada tusubiri miili mingine miwili kutoka Tanga ambayo majeruhi wengine wamefariki."amesema Mgumba.
Kutokana na kuongezeka idadi hiyo jumla ya marehemu kwa sasa wanafikia 21 ukiongeza na marehemu aliyekuwa akisafirishwa.
Chanzo - Mwananchi
Post a Comment