" MAPYA YAIBUKA AJALI YA KOROGWE, MADAKTARI WASIMAMISHWA KAZI

MAPYA YAIBUKA AJALI YA KOROGWE, MADAKTARI WASIMAMISHWA KAZI

 


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba ameunda kamati kuwachunguza madaktari wa wilaya hiyo pamoja na mganga mfawidhi Halmashauri ya Mji Korogwe na watasimamishwa kazi siku 14 ili kupisha uchunguzi kwa sababu za kuchelewa kufika kwenye tukio la ajali iliyouwa watu 18 Korogwe.

Mgumba amesema hayo jana, Jumamosi Februari 4, 2023 wakati akiongea na wafiwa waliofika chumba cha kuhifadhia maiti Korogwe kutambua miili na kusema kuwa lazima uchunguzi ufanyike kuhusiana na tukio la viongozi kushindwa kufika kwenye tukio kwa wakati.

"Serikali imeunda kamati ya siku 14 ili kufanya uchunguzi wa kina kutokana na daktari wetu wa wilaya DMO na daktari mteule wa hospitali hii ya wilaya, sababu ya kuchelewa kufika eneo la ajali. Imetokea saa 4:30 usiku wao wamefika saa 10 kasoro robo."  amesema Mgumba na kuongeza,


"Kitu hiki Serikali hatuwezi kukivumilia na hatuwezi kukisemea chini kwasababu wananchi wameona, waathirika wameona na wanajamii wameona. Serikali imekasirishwa na kitendo hicho na kusema kwa kuwa watumishi hao ni binadamu lazima wawape haki yao na itabidi  wasimame kwa siku 14 kupisha uchunguzi."

Akiongea baada ya kutembelea eneo la ajali akiwa na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Tanga, ambayo ameambatana nayo hadi hospitali ya mji wa Korogwe ambapo ndipo ilipo hifadhiwa miili ya marehemu mkuu wa mkoa amesema.

Aidha mkuu wa mkoa pia akatoa maagizo kwa mganga mkuu wa mkoa kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi hao huku akitoa wito kwa wananchi wa Korogwe na Mkoa wa Tanga kutojihusisha na wizi wa mali pale inapo tokea ajali.



Chanzo - Mwananchi

Post a Comment

Previous Post Next Post