" DC KAMINYOGE AKABIDHI BASKEL KWA WATOTO WENYE ULEMAVU ATAKA WAZAZI NA WALEZI KUWAJIBIKIA VYEMA MALEZI NA MAKUZI BORA

DC KAMINYOGE AKABIDHI BASKEL KWA WATOTO WENYE ULEMAVU ATAKA WAZAZI NA WALEZI KUWAJIBIKIA VYEMA MALEZI NA MAKUZI BORA

Na Elisha Petro, Misalaba Blog

Mkuu wa wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Aswege Kaminyonge amewakumbusha wazazi na walezi kuwajibikia vyema jukumu la malezi na makuzi bora ili kujenga jamii na taifa lenye maadili mema.

Ameyasema hayo kwenye hafla fupi ya kukabidhi baiskel zenye magurudumu matatu kwa watoto wawili wenye ulemavu wa viungo zilizotolewa na shirika la Cathoric Relief Service (CRS) ililiyofanyika katika shule ya Msingi Malampaka.

DC Kaminyonge amesema ni wajibu wa wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda watoto dhidi ya mazingira hatarishi hali ambayo itasaidia kuwa na taifa lenye kizazi chenye uadilifu.

Amewataka watoto hao, wazazi pamoja na walezi kuhakikisha wanatunza baiskel hizo ili ziweze kudumu.

Wakati huo huo amekumbusha wazazi na walezi kuwajibikia jukumu la kuchangia chakula shuleni kama njia sahihi ya kuweka mazingira wezeshi ya ufaulu wa wanafunzi.

Kwa upande wake Paroko wa Parokia ya Malampaka katika kanisa katoliki la Mama wa huruma Padre Renatus Mashenene ameshukuru na kupongeza juhudi za Askofu wa jimbo katoliki la shinyanga mhasham Liberatus Sangu kuliruhusu Shirika la Cartas kuendelea kushirikiana na jamii katika kutatua changamoto mbalimbali.

Kwa upande wao wazazi wa watoto waliopatiwa msaada huo wameshukuru uongozi shirika la Cathoric Relief Service (CRS), Uongozi wa kanisa Katorika la Mama wahuruma  pamoja na  uongozi wa serikali kwa ujumla   kwani ilikuwa ngumu kwao pekee kutatatua changamoto ya uapatikanaji wa baiskeli hizo.

Mkuu wa wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Aswege Kaminyonge akikabidhi baskel kwa mtoto wenye ulemavu wa viungo huku akiwa ameambatana na mama yake mzazi


Post a Comment

Previous Post Next Post