
Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mashirika mawili
yasiyokuwa ya kiserikali Mkoani Shinyanga Nancy Foundation na Ubongo learing
yameanza kutekeleza mradi wa kupunguza watoto wa mtaani unaoitwa “Home is where the heart is”.
Akizungumza kwenye hafla
maalum ya kutambulisha mradi huo Mkurugenzi na mratibu wa shirika la Nancy
Foundation katika programu ya marafiki wa watoto Bwana Ezra Manjerenga, amesema
hatua hiyo itasaidia kupunguza na badaye kutokomza kabisa watoto wa mtaani.
Amesema mradi huo
utatekelezwa kwa kipindi cha Miezi mitatu na kwamba utakuwa endelevu ukifanyika
kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Askari wa jeshi la akiba
mgambo Ezekia Isaka ambaye ameshirikiana na mashirika hayo kuwafikia watoto
wanaoishi mitaani ameeleza hali halisi ilivyo
“Tulikuwa
tunawakuta kwenye changamoto ya Stendi ya mabasi wanaomba omba wanakula vyakula
ambavyo havieleweki tulienda pia mtaa wa Ibinzamata tulifanikiwa kupata watoto
watano tukaja kupata tena watoto wengine maeneo ya relini watoto wengine tumekuja
kuwapatia hapa kata ya mjini”.amesema Mgambo Ezekia
Isaka
Misalaba Blog imezungumza
na baadhi ya watoto ambapo wametaja kuwa changamoto ya wazazi kutowapatia
mahitaji ya muhimu ikiwemo chakula na vifaa vya shule ndiyo chanzo ambacho
kinapelekea kukimbilia mitaani ikiwa lengo lao ni kwenda kuomba msaada hasa
chakula.
Baadhi ya maafisa
watendaji wa serikali walioshiriki katika zoezi hilo akiwemo Afisa
ustawi wa jamii Manispaa ya Shinyanga Ancila Katero, Afisa maendeleo ya jamii kata ya Mjini
Shinyanga Blandina Joseph Mwinamila pamoja na mtoa elimu kutoka Polisi dawati
la jinsia na watoto wametoa wito kwa wazazi na walezi
kusimamia vyema makuzi ya watoto ili kudhibiti ongezeko la watoto wa mitaani.
Jumla ya watoto 45 waliokuwa
wakiishi katika mazingira hatarishi kwenye mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Shinyanga
wamekusanywa na kupatiwa elimu ya malezi na maadili April 14,2023
Baadhi ya watoto wakipata chakula cha pamoja na mratibu wa shirika la Nancy Foundation katika programu ya marafiki wa watoto Bwana Ezra Manjerenga

Mkurugenzi na mratibu wa shirika la Nancy Foundation katika programu ya marafiki wa watoto Bwana Ezra Manjerenga akizungumza baada ya zoezi hilo kutamatika

Afisa maendeleo ya jamii kata ya Mjini Shinyanga Blandina Joseph Mwinamila akizungumza na Misalaba Blog baada ya zoezi hilo kutamatika
Post a Comment