Kwa wale waliopata kusoma historia au kusikia hadithi
za makabila, hasa ya Wasukuma na Wanyamwezi, hawakukosa kusikia habari ya
Ng’wanamalundi.
Misalaba Blog imefika na kuzungumza na baadhi ya jamii ya eneo hilo ambao wameeleza kuwa kaburi
la Ng’wanamalundi limejengwa kupitia uongozi wa serikali ya awamu ya sita
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu
Hassan.
Lengo la serikali lilikuwa ni kutambua mchango wa
Ng’wanamalundi kupitia uwezo wake aliokuwa nao ambapo inasemakana ni kweli
alikuwa namchango mkubwa katika jamii.
Mtu huyo aliyewahi kuutingisha utawala wa Wajerumani, alizaliwa katika ukoo wa
kawaida akiwa mcheza ngoma mashuhuri, mwaka wa kuzaliwa 1840 akiwa katika kijiji cha Seke Wilaya ya
Kishapu Mkoani Shinyanga alifariki dunia Februari 2 mwaka 1936.
Katika makala hii usahihi wa historia yake unaelezwa kuwa watu wengi walikuwa
wakimjadili kwa maoni tofauti, wengine wakimsifu kama shujaa huku wengine
wakihusisha uwezo wake na nguvu za giza.
Jina lake halisi halikuwa Ng’wanamalundi
bali lilikuwa Igulu Bugomola, ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Mwakubunga
Nera wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
Ng’wanamalundi alikuwa mtoto pekee wa kiume na wa mwisho kati ya wanne, kwa
baba yake Bugomola na mama yake, Ngolo Igulu.
Igulu (Ng’wanamalundi), alikuwa na tabia ya uzururaji
tangu utotoni na mara nyingi haikuwa rahisi kumkuta nyumbani alikuwa mashuhuri
kutokana na umahiri wake wa kucheza ngoma na mara nyingi alipokuwa akitembea
mitaani alifuatwa na kundi kubwa la watoto.
Hali ya kuchukiwa kwa Ng’wanamalundi ilienea pale kijijini kiasi cha kuanza
kumkebehi, hasa kutokana na umbo lake refu na miguu yake myembamba kuanzia
magotini hadi kwenye makanyagio, ikiwa mirefu kuliko kawaida.
Hali hiyo ilisababisha kumdhihaki na kumwongezea chuki zaidi kwa wanakijiji wa
eneo hilo waliodiriki kumtukana kwa lugha ya Kisukuma hapo ndipo ukawa mwanzo
wa kufutika kwa jina la Igulu na kuwa Ng’wanamalundi, jina ambalo lilitokana na
urefu wa miguu yake na kila kona walimuita hivyo.
Kadiri siku zilivyosonga mbele Ng’wanamalundi alizidi kujiimarisha katika
kikundi chake cha ngoma ambayo ilivuta vijana wengi, pia baadaye ilitumika kama
jeshi la kukodiwa na Watemi inapotokea vita.
Pamoja na wazazi kumchukia sana, lakini vijana walimpenda na kikundi chake
kikubwa cha ngoma kilipendwa na kutumika katika sherehe mbalimbali kwenye
familia za Kitemi za wakati huo.
Ng’wanamalundi na wenzake wawili walikwenda kwa bibi kizee mmoja kutafuta dawa
itakayowasaidia katika shughuli zao za kucheza ngoma, ambapo bibi kizee huyo
alikubali kuwasaidia.
Imeelezwa kuwa baada ya kusimama
aliamuru kila mmoja achimbe shimo lenye urefu hadi kiunoni, na baada ya
kukamilika kwa mashimo hayo aliwaambia wakusanye kuni na kuzitumbukiza.
Baada ya kazi hiyo kukamilika walipekecha moto na kuziwasha zile kuni na moto
uliposhika kasi aliwachukua wale vinyonga watatu na kuwawekea dawa mdomoni na
kisha aliwatupia ndani ya moto huo, wakateketea wote.
Ngw’anamalundi alikimbia akapanda juu ya mti, kifaru alifika kwenye shina la mti
na kuanza kuliparua kwa hasira na baadaye aliondoka kabla hajafika mbali
alimuona yule bibi kizee akikutana na faru huyo.
Ng’wanamalundi alishuhudia kifaru
akimrarua rarua bibi kizee mpaka akafa, kisha kifaru alitoweka kusikojulikana
huku akimuacha Ng’wanamalundi asijue la kufanya juu ya mti.
Ng’wanamalundi baada ya muda alishuka juu ya mti na kwenda kwenye maiti ya yule
bibi kizee, akaamua aibebe mgongoni airejeshe nyumbani, lakini kabla hajafika
mbali alisikia sauti ikisema, “Igulu bajahe abiyo akiwa na maana Igulu wenzako
wamekwenda wapi”.
Sauti hiyo ilimshtua Ng’wanamalundi ambaye alimshusha bibi kizee mgongoni mwake
na akashangaa kumuona akiwa hai asiyekuwa na jeraha lolote, kama alivyokuwa
baada ya kushambuliwa na faru.
“Igulu tujage ahante ugo waliwalinaga,
akiwa na maana Igulu twende kwenye mti uliokuwa umepanda, Ng’wanamalundi
aliongozana na bibi kizee huyo mpaka kwenye ule mti aliyachukua magamba ya mti
yaliyokuwa yameparuliwa na faru,”
Baada ya zoezi hilo kukamilika bibi kizee huyo alimtengenezea dawa aliyokuwa
akihitaji, na kisha Mwanamalundi alirejea kwao kuendelea na shughuli zake za
ngoma aina ya Kahena, ambayo mpaka leo inaendelea kwa baadhi ya maeneo jina
lingine ni Wigashe.
Ng’wanamalundi akiwa katika harakati zake za kujiimarisha katika masuala ya
dawa zake za ngoma, alienda kuchimba kwenye pori la Mwandutu huko wilayani
Maswa sasa ni Wilaya ya Kishapu, ambalo lilikuwa katika miliki ya Mtemi Chalya.
Imeelezwa kuwa baada ya kufika katika pori hilo akiwa na wafuasi wake
wakiendelea kuchimba dawa, ghafla alitokea Mtemi Chalya na kumuuliza; “Ubebe
nani wakuwilaga kwiza ngh’wiporu lyane” akiwa na maana; “Wewe nani amekuambia
kuja kwenye pori langu?”
Mwanamalundi alimjibu; “ Ubebe ulintemi wa banhu pye nu nene nding’wenekele wa
maporu pyee.” Akiwa na maana “Wewe ni Mtemi wa watu wote na mimi ni mmiliki wa
mapori yote”. Kauli hiyo ilimuudhi Mtemi Chalya.
Anasema, kufuatia kauli hiyo Mtemi Chalya aliita jeshi lake kwa lengo la kuja
kumkamata, lakini walishangaa baada ya kufika katika eneo waliloelezwa na Mtemi
wao kuwa Ng’wanamalundi anatakiwa kukamatwa na kuuawa, lakini walishindwa baada
ya kukuta simba wengi sana.
Jeshi hilo na Mtemi ilibidi kukimbia kujiokoa kwani simba hao walianza
kuwashambulia, wengine walitawanyika ovyo na baadhi yao wachache tu ndiyo
walionusurika.
Lakini cha kushangaza walipofika walimkuta Ng’wanamalundi na wafuasi wake
wakimalizia kula chakula nyumbani kwa Mtemi Chalya, ambaye hata yeye
alichanganyikiwa na kushindwa kuongea lolote.
Ng’wanamalundi baada ya kumaliza kula chakula kwa Mtemi Chalya aliondoka na
wafuasi wake na akapitia kwenye lile pori akachimba dawa zake na kuondoka kwenda
kuendelea na maisha yake.
Katika ngoma zake; Ng’wanamalundi alikuwa na tabia ya kuwatahadharisha
mashabiki wake kuacha kwenda wakiwa wamejipaka dawa yoyote ile, anasema.
Aliwaambia: “Bing’we akwiziza munho wibilaga bugota bosebose ulu kutora akotora
henaha,ulo nsabo akupandika heneha.”
Kauli hiyo ilikuwa na maana nyie asije mtu amejipaka dawa yoyote hapa kama ni
kuoa, ataoa hapahapa kama ni mali atapata hapahapa, hata hivyo kuna wale
walipuuza kauli hiyo kwa kuja wamejipaka dawa kwa lengo la kujipima uwezo wa
dawa zao. Lakini hawakufanikiwa na badala yake walikufa.
Akiwa anaendelea na ngoma yake wananchi wa Kijiji cha Sekke waliibiwa ng’ombe
wengi sana na watu kutoka Kabila la Wamasai ambao walienda kuwahifadhi katika
Pori la Mwanima karibu na Kijiji cha Bubiki.
Ng’wanamalundi na kikosi chake waliondoka Wilaya ya
Kwimba mkoani Mwanza na kuelekea Sekke wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kwa
lengo la kusaidia kuzikomboa ng’ombe zilizoibwa. Hata hivyo kabla hawajafika
uwanja wa vita, Ng’wanamalundi alifanya utabiri wake uliotokana na nguvu ambazo
alizipata kutoka kwa Bibi Kizee wa porini.
Aliwaambia kuwa
kabla ya vita, itatokea mvua kubwa sana na ikikatika watakuja ndege hai aina ya
mwewe watakaokuwa wanazungukazunguka kwenye zile ng’ombe na hapo sasa wafuasi
wake wakate miti mifupi mifupi (Lubugu).
Utabiri huo ulitimia, kwani mvua ilinyesha kubwa sana na baada ya kukatika wale
mwewe walijitokeza wengi sana wakawa wanazunguka kwenye zile ng’ombe na ndipo
yale mapigano ya Wamasai na wafuasi wake yalipoanza.
Aliwaeleza kuwa baada ya kuwa na fimbo ya Lubugu wale
wenye upinde na mishale watakaa nyuma na kazi yao watakuwa wanazipiga zile ngao
za Kimasai na zikidondoka chini ndipo wenye pinde na mishale waanze
kushambulia.
Mwanamalundi alipigana hiyo vita ya Wamasai mpaka
akazirejesha zile ng’ombe na aliwatokomeza Wamasai mpaka kwenye mpaka wa Mto
Manonga unaotenganisha Tinde Shinyanga na Nzega mkoani Tabora.
Hapo ndipo
ilibainika Wamasai hao walikuwa wametumwa kuiba ng’ombe Usukumani na Mtemi
Tinginya wa Busongo Nzega, ambapo baada ya vita hiyo Ng’wanamalundi na kundi
lake walirudi Sekke na kupewa jina la Kishosha Mang’ombe tafsiri ikiwa ni
mrudisha ng’ombe. Baada ya vita hiyo Ng’wanamalundi alirudi nyumbani kwao
wilayani Kwimba kuoa, lakini bahati mbaya ilimkuta, kwani kila mke
aliyejifungua, mtoto alikufa.
Baba yake Bugomola akaenda Ntuzu kwa sasa Bariadi kufanyiwa tambiko kuhusu
uzazi kwa mwanaye. Akiwa huko Ntuzu, Bugomola alielezwa mwanaye Ng’wanamalundi
hatapata mtoto kwa wake zake alionao.
Hivyo aoe msichana atakayempata upande wa Mashariki
ambaye atakuwa akiitwa Nkamba na atazaa watoto watatu; wa kwanza ataitwa Sitta,
wa pili Ngassa na wa tatu Marieta.
Baada ya kurudi Bugomola, haikumchukua muda mwanaye
Ng’wanamalundi akapata msichana akaoa na akaendelea na shughuli yake ya
kuendesha kikundi cha ngoma.
Ng’wanamalundi kuwekwa kizuizini Akiwa anaendelea na
ngoma zake katika maeneo ya Kanda ya Ziwa, siku moja yeye na kikundi chake
walipokuwa wakiburudisha katika maeneo ya Bukumbi mkoani Mwanza, wafuasi wake
walipumzika kwenye mti mkubwa ambapo pia kilikuwa Kituo cha Wajerumani,
Ng’wanamalundi aliwaambia wafuasi wake waondoke waende kwenye ngoma, wafuasi
wake waligoma wakadai wanapumzika kwenye kivuli hicho ili wavute sigara.
Baada ya kuwabembeleza vya kutosha akabaini hawataki
kumsikiliza ndipo alipounyooshea kidole ule mti akisema “Ngh’walemelaga hanti
gunugo aliyo gumaga,” akiwa na maana “Mmekatalia kwenye mti huo huku ukiwa
umekauka.” Ghafla mti huo wote ulikauka.
Kuona hivyo wafuasi wake wakaondoka wote kwenye huo mti wakaenda kuendelea na
ngoma yao ambayo walicheza katika eneo la Bukumbi na Busagara karibu na Mji wa
Mwanza na walipomaliza walirejea Kwimba.
Akiwa Kwimba alicheza ngoma moja na Gindu Nkima, ngoma
hiyo ilikuwa ngumu kwake ilichezwa sehemu za Mwanagwa.
Baada ya kuwa
amezidiwa Ng’wanamalundi, wapishi wake walimfuata na kumtaka awasaidie namna ya
kupata kuni za kupikia. Kutokana na uharaka aliokuwa nao Ng’wanamalundi
alielekeza kidole chake kwenye miti ya minyaa iliyokuwa mbele yake huku akisema
“Batemagi pye abenababa mkazugile,” akiwa na maana “Yakateni yote haya mkapikie.”
Baada ya kauli
hiyo minyaa yote ilikauka na kuwa kuni na wafuasi wake walikata wakaenda
kupikia chakula akiwa katika ngoma hiyo wakati huo barabara ya kutoka Shinyanga
kwenda Mwanza ilikuwa inachongwa na manamba waliokuwa wakikamatwa na Wajerumani
kwa ajili ya kazi hiyo, Gavana wa Kijerumani wa eneo la Mwanza alipita eneo
hilo akiwa amepanda punda alikuta kazi imesimama, alipohoji kwanini kazi
imesima alielezwa wananchi wote wamekwenda kwenye ngoma ya Ng’wanamalundi.
Kitendo hicho kilimchukiza sana Mjerumani huyo, ambaye
aliondoka akaenda Mwanza na baada ya siku mbili walikuja askari waliomkamata
Ng’wanamalundi na kumfunga mnyororo na watuhumiwa wengine walipelekwa Mwanza na
kuwekwa gerezani.
Kosa hilo kwa utawala wa Ujerumani lilihesabiwa kuwa ni uhaini wa kupinga
utawala wao hivyo alitakiwa kupewa adhabu ya kunyongwa. Kabla hajapelekwa
Mwanza, kwa kuwa ilikuwa ni safari ya kwenda kunyogwa, alipelekwa nyumbani kwa
wazazi wake kuaga.
Alipofika nyumbani kwao alimpa mama yake shoka
aliloliweka pembezoni mwa ukuta chumbani na maziwa, huku akitoa maelekezo.
“Mayu imbasa yeneye ulu yulina ng’wigulya mumhonatwalwa ulu yika hase
mumhonashoka amabele genaya ulu guganda mumhonacha, ulu gita lububhi
mumhonasata.” akiwa na maana hii shoka ikipanda juu basi nitakuwa nimepelekwa
ikishuka chini nitakuwa nimerudishwa.”
Ng’wanamalundi
aliendelea kumpa maelekezo mama yake kuwa haya maziwa yakiganda atakuwa amekufa
na pindi yakipata utando atakuwa anaumwa, baada ya maelezo hayo Ng’wanamalundi
alipelekwa Mwanza gerezani ambako alikutana na Mtemi Makongoro wa Mwanza.
Siku iliyofuata walitolewa wote ambapo walikutana pia
na mganga aliyemtabiria kuzaa watoto watatu ambaye naye alikuwa amekamatwa kwa
kosa la kupiga ramli iliyosababisha mauaji ya kishirikina.
Asubuhi kila mmoja alisomewa mashtaka yake ambapo Ng’wanamalundi alisomewa
mashtaka matatu, shtaka la kwanza kuukausha mti uliokuwa ukitumiwa na maofisa
wa utawala wa Wajerumani kama kituo cha kupumzikia huko Bukumbi Mwanza.
Shtaka la pili kuwatungia na kuwaimbia nyimbo mbaya
Wajerumani na la tatu ni kukwamisha ujenzi wa Barabara ya Mwanza kwenda
Shinyanga.
Ng’wanamalundi alidaiwa kuchezesha ngoma eneo la
Mwanangwa hali iliyosababisha wafanyakazi wa manamba waliokuwa wakilima
barabara hiyo kuacha na kwenda kuangalia ngoma yake hali iliyowachukiza
Wajerumani.
Kaburi la Ng'wanamalundi likiwa limejengelewa mwonekano wa nyumba
Kaburi la Ng'wanamalundi likiwa limejengelewa mwonekano wa nyumba
Holo Bunzali ambaye ni ndugu yake na Ng'wanamalundi wakati akiwa ni mmoja ya waliopata nafasi ya kuzungumza na Misalaba Blog
Post a Comment