Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Serikali imesema kuwa ili
kuondoa changamoto ya watoto kuishi katika mazingira hatarishi mitaani, ipo
haja kwa wazazi na walezi kuwajibikia vema jukumu la malezi na makuzi bora.
Kauli hiyo imetolewa na
Afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Ansila Materu baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwakabidhi katika familia zao watoto wanne
waliokuwa wakiishi mitaani shughuli ambayo ilifanyika kwa kushirikiana na mashirika
mawili yasiyokuwa ya kiserikali Mkoani Shinyanga Nancy Foundation na Ubongo
learing.
Afisa
ustawi wa jamii huyo Bi. Ansila Katero ametaja baadhi ya sababu
zinazochangia watoto kutoroka nyumbani
kwa wazazi au walezi wao kuwa ni pamoja na kukosa mahitaji muhimu ikiwemo chakula.
Amesema zoezi la
kuwarejesha watoto kwenye familia zao litakuwa endelevu katika Manispaa ya
Shinyanga.
“Tunashukuru
zoezi letu na kutambua watoto wanaozurula mitaani lipo katika hatua nzuri ni
siku ya pili tumefanya zoezi hili kwa siku ya kwanza tulipata watoto kumi na
nane (18 ) leo tumefanikiwa kuongeza watoto sita (6) na watoto wanne (4) tumebahatika kuzungumza
na wazazi wao na kuwasihi ili tuweze
kupata suluhisho la kuwasaidia watoto hawa”.
“Ila
tulichogundua katika zoezi hili kinachosababisha asilimia kubwa watoto kutoroka
nyumbani ni ile hali ya wazazi kuwa bize na shughuli zao kwahiyo hawana muda wa
kukaa na watoto”
“Kwahiyo
tunawasihi wazazi wawe karibu na watoto wawafuatilie watoto mashuleni pia
wanapotoka nyumbani wahakikishe wanaacha chakula kwa ajili ya watoto kwa sababu
changamoto wanasema wanaenda mitaani kwa ajili ya kutafuta chakula lakini pia
wazazi tuwapangia watoto kazi za kufanya ili wasiende kuzurula”.amesema
Afisa ustawi Ansila
Baadhi ya wazazi na
walezi waliokabidhiwa watoto wao waliokuwa wakiishi mtaani wameshukuru na
kupongeza juhudi za serikali kwa kushirikiana na mashirika hayo mawili Nancy
Foundation na Ubongo learing kutekeleza mradi huo unaolenga kuwaondoa watoto
wanaokimbilia mitaani.
Mashirika hayo mawili
Nancy Foundation na Ubongo learing yanatekeleza mradi wa Miezi mitatu unaolenga
kupunguza au kumaliza kabisa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani katika
Manispaa ya Shinyanga.
Shirika la Nancy Foundation na Ubongo learing kwa
kushirikiana na serikali ( Maafisa ustawi wa jamii Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga) wakiwa kwenye mazungumzo ya pamoja na mzazi wa mtoto katika kata ya
Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
Afisa
ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Lemiflora Nyalaja akizungumza
ni mmoja wa watoto waliorejeshwa nyumbani kwa wazazi wao katika Manispaa ya
Shinyanga.
Post a Comment