Na Moshi Ndugulile
Wajumbe wa kamati ya watumiaji wa huduma ya nishati na Maji RCC Mkoa wa Shinyanga wamefanya ziara katika baadhi ya Shule za sekondari na vyuo katika Manispaa ya Shinyanga.
Ziara hiyo ni oparesheni elimisha vijana mashuleni kuhusu majukumu ya taasisi hiyo,haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za nishati na maji,lakini pia kufahamu umuhimu wa matumizi sahihi ya nishati na maji
Baadhi ya shule zilizotembelewa na wajumbe hao ni pamoja na Shule ya sekondari Old shinyanga, Shule ya wasichana ya Shinyanga, town sekondari na chuo cha ufundi stadi VETA, ambapo wanafunzi wametakiwa kuwa mabalozi wazuri wa kufikisha ujumbe mzuri kwa wengine kuhusu EWURA CCC na majukumu yake lakini pia kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji wa nishati na maji pamoja na matumizi sahihi ya nishati na maji.
Akizungumza na wanafunzi katika shule ya sekondari ya wasichana ya Shinyanga mjumbe wa kamati hiyo Bi Mariam kifungu Mrisho amewataka wanafunzi hao kuwa mabalozi wa matumizi sahihi ya maji na nishati ili kuepuka gharama kubwa ya fedha za kulipia bidhaa hizo.
Kamati hiyo ina jumla ya wajumbe watano wakiongozwa na mwenyekiti Bwana Jonathan Manyama, Mwalimu Zezema Shilungushela, Joseph Ndatala,Mariam kifungu pamoja na Moshi Ndugulile.
Wakiwa katika chuo cha ufundi stadi VETA Mkoa wa Shinyanga Mkuu wa chuo hicho ameishukuru na kuipongeza RCC Mkoa wa Shinyanga ambapo amesema ziara hiyo italeta mabadiliko kwa vijana hao na jamii nzima ya Chuo hicho kuondokana na matumizi yasiyo sahihi ya nishati na maji,changamoto ambayo imekuwepo kwa muda mrefu na kuwasababishia gharama kubwa
Jumla ya wanafunzi 3020 na walimu 72 kutoka shule tatu na chuo kimoja zilizotembelewa na kamati ya watumiaji wa huduma ya nishati na maji ya Mkoa wa Shinyanga RCC wamepata elimu juu ya matumizi sahihi ya maji na nishati.
Post a Comment