Juhudi za kumtafuta mtoto Salum Mathew aliyesombwa na mto
Mhumbu zinaendelea baina ya Jeshi la zimamoto na uokoaji kwa
kushirikiana na wananchi wa kata ya Ndembezi ikiwa ni siku ya tatu
tangu kuanza kwa zoezi hilo.
Mkuu wa Jeshi hilo Inspekta Stanley Luhwago amesema kuwa leo asubuhi
walipokea taarifa za kuonekana mtu kando kando ya mto Mhumbu kijiji
cha ikoma kata ya Itilima lakini walipofika kuutambua mwili huo
walibaini kuwa hakuwa Salum kwa hiyo wameendelea na zoezi la
utafutaji.
“Asubuhi tukiwa tunaendelea na zoezi tulipata taarifa kwamba karibia
na Kishapu kuna mtoto wamepatikana akiwa amepoteza maisha lakini
tukafuatilia huko ikaonekana ni kwamba kweli tukio lilikuwepo lakini
alikuwa ni mtoto wa kulekule na wameshazika tayari kwahiyo tukarudi
kuendelea na zoezi la kumtafuta Salum mpaka sasa bado hatujafanikiwa
kumpata”.amesema Inspekta Luhwago
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Tambukareli kata ya
Ndembezi Bwana Japhet Kisusi amesema bado hawajafanikiwa kumpata
mtoto huyo hali iliyomlazimu kupiga la mgambo kwa ajili ya shughuli
hiyo ambayo ameitaja kuwa na changamoto kutokana na mazingira
hatarishi ya mto huo.
“Changamoto iliyopo kuna sehemu korofi ambazo mtu anahofia
usalama wake kuingia pale na maji ya mto huu ni machafu sasa wale
maaskari inawalazimu wazame kwenye maji yale na wananchi wenye
mapenzi mema lakini kuna sehemu zingine ni hatarishi kuna vichaka
kuna miba humo kuna miti iliyosimama hovyo lakini mtu inapigi azame
sasa wangekuwa na vifaa vya kuzamia majini walau ingeleta
afadhari”.amesema Mwenyekit Japhet
Leo ni siku ya tatu tangu mtoto Salum Mathew aliposombwa na Maji ya
mto Mhumbu wakati akiogelea Jumamos Februari 3,2024.
Salum ni mkazi wa mtaa wa Mbuyuni kata ya Ndembezi Manispaa ya
shinyanga, ambaye anasoma Darasa la Nne katika shule ya Msingi
Bugoyi B.
TAZAMA VIDEO YA MWENYEKITI WA MTAA WAKATI AKIZUNGUMZA JANA FEBRUARI 4,2024
Post a Comment