" MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AWASISITIZA WANANCHI KUTUMIA FURSA HII KUFIKISHA KERO NA CHANGAMOTO ZAO ILI ZISHUGHULIKIWE HARAKA

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AWASISITIZA WANANCHI KUTUMIA FURSA HII KUFIKISHA KERO NA CHANGAMOTO ZAO ILI ZISHUGHULIKIWE HARAKA


TAZAMA VIDEO

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kesho anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi katika Halmashauri tatu za Manispaa ya Shinyanga,Kahama na Msalala

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumanne Februari 27,2024 amesema ziara hiyo pamoja na mambo mengine imelenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi kupitia mikutano ya hadhara katika Halmashauri hizo.

Ameeleza kuwa kesho Februari 28,  ziara yake itaanzia katika Manispaa ya Shinyanga ambapo atafanya Mkutano wa hadhara  katika kata ya Mjini, kuanzia saa tano asubuhi na kwamba Alhamis Februari 29, kuanzia majira ya saa tano asubuhi atakuwa katika Manispaa ya Kahama.

RC  Mndeme amesema Machi mosi, 2024  atazungumza na wananchi wa Halmashauri ya Msalala kupitia Mkutano wa hadhara  ambapo saa tano asubuhi atafanya Mkutano wa hadhara katika kata ya Kakola, na baadaye Saa nane mchana atazungumza na wananchi wa kata ya Segese.

Ametoa rai kwa Wananchi wote wa maeneo atakayofanya ziara kuhudhuria katika mikutano ha hadhara ili waweze kuwasilisha kero zao,pamoja na kutoa ushauri na maoni.

Post a Comment

Previous Post Next Post