Taasisi ya kuthibiti
ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) imetoa Elimu kwa wananchi hasa wakulima Mkoani
Shinyanga kupitia Misalaba Media, juu ya umuhimu wa wakulima kuacha kilimo cha
mazoea na badala yake kutumia mbegu bora
ili kuchochea kilimo Biashara chenye tija.
Afisa uthibiti ubora wa
mbegu Bi. Zera Mwamkemwa amesema Elimu hiyo ni sehemu ya mpango endelevu wa
uelimishaji wa makundi mbalimbali wakiwemo wakulima kuhamasisha matumizi ya
mbegu bora ili waweze kulima kilimo chenye tija.
Mwamkemwa amesema elimu
hiyo ya matumizi ya mbegu bora itakuwa chachu kwa wakulima kulima kilimo chenye
tija ikilinganishwa na awali ambapo walikuwa wakipata mavuno kidogo kutokana na
kutumia mbegu zisizokuwa na ubora.
Kwa upande wake Afisa
Mkaguzi wa mbegu taasisi ya kuthibiti ubora wa mbegu Tanzania TOSCI, Bwana Joseph
Pagu amesisitiza wafanyabiashara wenye maduka ya mbegu kufuata kanuni za mbegu
kwa mujibu wa sheria ili kumfikishia mkulima mbegu bora.
Amezitaja baadhi ya
changamoto wanazozibaini wakati wa zoezi la ukaguzi kwenye maduka ya mbegu ikiwemo
ile ya mkulima kutochukua stakabadhi ya mauzo.
Post a Comment