" ASKOFU SANGU ASISITIZA JAMII KUZINGATIA HAKI ZA YATIMA NA WAJANE

ASKOFU SANGU ASISITIZA JAMII KUZINGATIA HAKI ZA YATIMA NA WAJANE

 

Jamii imeaswa kuwatendea haki na kuwasaidia yatima na wajane, badala ya kuendelea kuwanyanyasa kupitia mali zinazoachwa na marehemu pale Baba wa familia anapofariki dunia.

Rai hiyo imetolewa leo na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhahashamu Liberatus Sangu, wakati wakiwahubiria waamini kupitia Ibada ya Ijumaa kuu, iliyofanyika katika Kanisa kuu la Mama mwenye huruma Ngokolo mjini Shinyanga.

Askofu Sangu ameeleza kutofurahishwa na tabia ya ndugu wa marehemu hasa pale baba wa familia anapofariki dunia kugeuza msiba kama sehemu ya kwenda kuhakiki mali alizoziacha ili wazigawane bila kujali wategemezi aliowaacha, akiwemo mjane na watoto.  

Ameitaka jamii kuhakikisha suala la haki za yatima na wajane linazingatiwa badala ya kuwa na mawazo hasi ya kugawana mali za marehemu bila kujali familia aliyoiacha.

Kauli ya Askofu Sangu inakuja wakati kukiwa na migogoro mingi ya kugombania mali ikiwemo mashauri ya mirathi yasiyoisha katika Mahakama mbalimbali, hali ambayo imesabisha uhasama mkubwa  kati ya wazazi au ndugu wa marehemu, watoto na wajane wa marehemu.

Katika hatua nyingine, Askofu Sangu amewataka Wakristo kuendelea kumwongokea Mwenyezi Mungu kwa kutubu dhambi zao mara kwa mara, pamoja na kuacha roho ya vivu ambayo ni chimbuko la chuki na mateso kwa wengine.

Amewakumbusha umuhimu wa kuombana msamaha na kusameheana huku akibainisha kuwa, familia na ndoa haziwezi kudumu endapo hazitajengwa katika msingi wa msamaha.

Leo, Wakristo kote ulimwenguni wameshiriki Ibada ya Ijumaa kuu, ambayo ni kumbukumbu ya mateso na kifo cha Yesu kristo.

Maandamano ya kuingia Kanisani kwa ajili ya Ibada

Askofu Sangu (katikati) Paroko wa Parokia ya Ngokolo Padre Adolf Makandagu (wa kwanza kulia) na Shemasi James Chingila (wa mwisho) wakiwa wamejilaza kifudifudi ikiwa ni ishara ya kujinyenyekeza kwa Yesu aliyeteswa na kufa msalabani kwa ajili ya dhambi za wanadamu

Msomaji wa somo la kwanza akisomo wakati wa Ibada

Wanakwaya wa Kwaya ya Mt.Joseph mfanyakazi wakiimba kwenye Ibada

Msomaji wa somo la pili akisoma somo

Shemasi James Chingila na baadhi ya Wanakwaya wakisomo Historia ya mateso ya Yesu

Askofu Sangu akitoa Homilia


Walelewa wa Shirika la kijimbo la Maria Mtakatifu Mama wa Huruma wakiwa kwenye Ibada ya Ijumaa kuu

Waamini wakiwa kwenye ibada

Shemasi James Chingila na watumikiaji wakileta Msalaba kwa ajili ya Ibada ya kuabudu Msalaba

Shemasi Chingila akionyesha Msalaba kwa waamini

Wanakwaya

Waamini wakiabudu Msalaba

Askofu Sangu akiwakomunisha waamini

Shemasi Chingila akiwakomunisha waamini

Post a Comment

Previous Post Next Post