" MKUU WA WILAYA YA KAHAMA MHE. MHITA AWATAKA WATUMISHI WA AFYA HALMASHAURI YA USHETU KUTUMIA LUGHA NZURI KUWAHUDUMIA WANANCHI

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA MHE. MHITA AWATAKA WATUMISHI WA AFYA HALMASHAURI YA USHETU KUTUMIA LUGHA NZURI KUWAHUDUMIA WANANCHI

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mheta akizungumza kwenye mkutano wa hadhara kata ya Nyamilango.Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaWatumishi wa idara ya Afya katika Halmashauri ya Ushetu  Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kutumia lugha nzuri wakati wa kutoa huduma na kufuata taratibu na kanuni za aAya ili kuondokana na baadhi ya malalamiko ya wananchi pamoja na kutoa huduma iliyobora.Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. MBONI MHITA katika mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji cha Mitonga kata ya Nyamilango, ambapo amesema wananchi wanapaswa kuhudumiwa vizuri kwa utaratibu na miongozo ya sekta ya afya na pasipo kutozwa fedha kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano pamoja na watumishi kutumia lugha nzuri.Kwa upande wao, baadhi ya wakazi wa kijiji cha mitonga katika kata hiyo, RICHARD DAUD na ELIZABETH PASCHAL wakitoa kero zao kwa mkuu wa wilaya ya Kahama, wamesema wamekuwa wakitozwa fedha katika huduma za watoto chini ya miaka 5 pamoja na wakinamama wajawazito, huku wakimuomba MBONI kuwasaidia changamoto hiyo inayowakabili wakati wakipatiwa huduma.Kaimu mganga mkuu wa  Halmashauri ya Ushetu wakati akijibu kero hizo zilizotolewa na wananchi hao, ALPHONCE MALUNDE amesema kuwa wananchi wanapopata changamoto hiyo wawasiliane na ofisi ya mganga mkuu pamoja na kuwaomba washirikiane katika changamoto hiyo ili kuondoa malalamiko hayo kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.Hata hivyo, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ushetu HADIJA KABOJELA, amewataka wakinamama wajawazito kutojifungulia nyumbani na badala yake wafike katika zahanati, vituo vya afya na hospital ili kuondokana na matatizo mbalimbali ya kiafya pamoja kuepukana na vifo vya mama na mtoto.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post