" ASKOFU SANGU KESHO KUONGOZA MISA YA DOMINIKA YA HURUMA YA MUNGU NKOLOLO BARIADI MKOANI SIMIYU

ASKOFU SANGU KESHO KUONGOZA MISA YA DOMINIKA YA HURUMA YA MUNGU NKOLOLO BARIADI MKOANI SIMIYU

 Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, kesho ataongoza Misa ya Dominika ya huruma ya Mungu katika kituo cha kijimbo cha hija ya Huruma ya Mungu, kilichopo Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Nkololo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.

Kwa mujibu wa katibu wa Askofu Padre Paul Mahona, Misa hiyo itaanza saa 4:00, asubuhi na itahudhuriwa na Mapadre, watawa na waamini kutoka sehemu mbalimbali za Jimbo.
Dominika ya huruma ya Mungu huadhimishwa kila mwaka siku ya Jumapili ya pili ya Pasaka, ikiwa ni sehemu ya kufanya tafakari ya kina juu ya huruma ya Mwenyezi Mungu kwa wanadamu.
Dominika ya huruma ya Mungu huhitimisha kipindi cha siku kadhaa cha hija ya huruma ya Mungu, ambapo waamini kwa kushirikiana na viongozi wao wa kiroho hupata nafasi ya kushiriki mafungo na kusali kwa nia mbalimbali.

Post a Comment

Previous Post Next Post