Na Mapuli Kitina Misalaba
Wizara ya Ardhi imefanya
mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi unaotarajiwa
kuanza utekelezaji wake Julai mosi Mwaka huu 2024 kwenye kata 9 za Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga katika awamu ya kwanza.
Mgeni rasmi katika mkutano huo ni katibu tawala wa
Wilaya ya Shinyanga Bwana Said Kitinga akimwakilisha mkuu wa Wilaya hiyo Wakili
Julius Mtatiro.
Wakati akifungua mkutano huo Bwana Kitinga pamoja na
mambo mengine amewasisitiza wasimamizi wa mradi huo kutekeleza majukumu yao kwa
weledi, haki na usawa ili kuepusha migogoro kwa wananchi.
Pia amehimiza wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga ambao watafikiwa na mradi huo
kutoa ushirikiano ili malengo ya serikali yaweze kufikiwa katika kuimarisha
Wizara ya Ardhi.
‘Nawaomba
mchukue kama fursa kwenu na kutoa ushirikiano thabiti ili kufanikisha utekelezaji
wake, maeneo mengi yalitamani kupata fursa hii lakini kutokana na uchache wa
rasilimali hawakufanikiwa kufikiwa na mradi’.
“Nashauri
itumieni fursa hii kikamilifu kwa maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga na Mkoa wetu wa Shinyanga kwa ujumla, uboreshaji wa milki wa Ardhi
katika Wilaya utaleta matokeo chanya katika kuchochea maendeleo ya Wilaya ikiwa
ni pamoja na kuleta usalama wa milki za Ardhi, kukuza uchumi na kupunguza au
kumaliza migogoro itokanayo na Ardhi”.
“Mtakaopata
fursa ya kushiriki moja kwa moja katika utekelezaji wa mradi huu kwa kufanya au
kushauri serikali, nawaomba mfanye kazi kwa uaminifu na uadilifu wa hali ya juu
kwa kuzingatia uzalendo (Taifa kwanza) nawaomba wote tuwe wamoja tusemezane
ndani kwa ndani tuyarekebishe yale ambayo yanaweza kutia dosari katika mradi lakini
pia msifumbe macho wala kusita kuwasiliana na ofisi yangu kwa mambo
yanayohitaji kuboreshwa ili kuifanya Halmashauri yetu kupata matokeo chanya”Amesema
Kitinga
“Nafurahi
kutamka kuwa mkutano huu wa wadau wa mradi wa kuboresha usalama wa milki za Ardhi
Nchini unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga nimeufungua
rasmi”.
Kwa upande wake afisa mipango miji akimwakilisha
meneja urasimishaji mjini, Bwana Paulo Kitosi ameeleza hatua mbalimbali za
utekelezaji mradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo amesema kwa
awamu ya kwanza kata 9, vijiji 15 na vitongoji 21 vitanufaika na mradi wa
uboreshaji usalama wa milki za Ardhi.
Bwana Kitosi amesema mradi huo pia utakwenda sanjari
na utatuzi wa migogoro ya Ardhi ambapo ameeleza kuwa mradi huo utasaidia
kuimarisha makazi yasiyorasimi pamoja na kuongezeka usalama wa miliki katika
jamii.
Katika mkutano huo yamefanyika majadiliano ya pamoja
ambapo Afisa maendeleo ya jamii Bi. Tumaini Setumbi ametaja baadhi ya maazimio
yaliyofikiwa katika mkutano huo.
“Azimio
la kwanza ni utekelezaji wa mradi uanze mapema ili elimu iliyotolewa
isisahaulike azimio la pili ni wananchi kupewa elimu zaidi kuhusu umiliki wa
ardhi katika maeneo yenye madini lakini pia azimio lingine ni mradi kuajili
vijana waliomaliza vyuo walioko katika maeneo yanayofikiwa na mradi”
ametaja Setumbi
Bi. Setumbi awali wakati akiwasilisha yake ya
usimamizi wa masuala ya mazingira na jamii amesema katika mradi wa uboreshaji
usalama wa milki za Ardhi zipo miongozo mbalimbali ili kuhakikisha kuwa masuala
ya mazingira na jamii yanazingatiwa ambapo pia amesema upo mpango wa kutambua
makundi maalum.
Mradi huu umelenga kuboresha usalama wa milki za
Ardhi kwa kupanga, kupima na kusajili milki za Ardhi zipatazo 2.5
zinazojumuisha hati milki 1,500,000 na leseni za makazi 500,000 katika maeneo
ua mijini na hati za hakimiliki za kimila 500,000 vijijini ambapo Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga inakusudiwa kutoa hati milki zipatazo 62,200 katika
maeneo ya vijiji 15.
Mradi huu pia umelenga kusimika mfumo unganishi wa
kielekroniki wa kuhifadhi kumbukumbu za Ardhi (ILMIS) katika ofisi zote za
Ardhi za Mikoa za Halmashauri mbalimbali.
Tanzania inajumla ya Halmashauri 185 kati ya Halmashauri
hizo, Halmashauri zaidi ya 60 zinazotarajiwa kunufaika na mradi huu mjini na
vijijini ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ni miongoni mwa wanufaika
katika mradi huo.
Baadhi ya
kata ambazo zitanufaika na mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi katika
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ni pamoja na kata ya Samuye, Isela, Tinde, Didia,
Solwa, Salawe, Mwakitolyo, Iselemagazi, Mwenge pamoja na kata ya Usanda.
Mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa
milki za Ardhi umehudhuriwa na viongozi wa serikali na taasisi binafsi,
viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini, wawakilishi
kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, kamati ya ulinzi na usalama Wilaya
ya Shinyanga, madiwani wa Halmashauri hiyo kutoka kata mbalimbali, wakuu wa
divisheni na vitengo, wataalam kutoa Wizara ya ardhi makao makuu, wawakilishi
wa makundi maalum, viongozi wa kimila na wazee maarufu.
Mgeni rasmi, katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga
Bwana Said Kitinga akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji
usalama wa milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Juni 28,2024.
Mgeni rasmi, katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga
Bwana Said Kitinga akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji
usalama wa milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Juni 28,2024.
Afisa mipango miji akimwakilisha meneja urasimishaji
mjini, Bwana Paulo Kitosi akiwasilisha mara ya hatua mbalimbali za utekelezaji mradi katika
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa awamu ya kwanza, leo Juni 28,2024.
Afisa mipango miji akimwakilisha meneja urasimishaji mjini, Bwana Paulo Kitosi akiwasilisha mara ya hatua mbalimbali za utekelezaji mradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa awamu ya kwanza, leo Juni 28,2024.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Mhe. Ngassa Mboje awali akitoa salamu zake katika mkutano wa wadau wa mradi wa
uboreshaji usalama wa milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo
Juni 28,2024.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini Mhe. Edward Ngelela awali akitoa salamu zake katika mkutano wa wadau wa mradi wa
uboreshaji usalama wa milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo
Juni 28,2024.
Mwakilishi wa ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Solwa, ambaye ni Diwani wa kata ya Iselamagazi Mhe. Isack Sengerema awali akitoa salamu kutoka ofisi ya Mbunge katika mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Juni 28,2024.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga Bwana Edward Maduhu akisoma taarifa ya mradi wa uboreshaji
usalama wa milki za Ardhi amapo
ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuanzisha mradi huo ambao utasaidia
kutatua kero za Ardhi katika Halmashauri hiyo.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bwana Edward Maduhu akisoma taarifa ya mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi amapo ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuanzisha mradi huo ambao utasaidia kutatua kero za Ardhi katika Halmashauri hiyo.
Afisa mipango miji akimwakilisha meneja urasimishaji
mjini, Bwana Paulo Kitosi akiwasilisha mada inayosema usimamizi wa masuala ya
mazingira na jamii leo Juni 28,2024 katika mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji
usalama wa milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Afisa mipango miji akimwakilisha meneja urasimishaji mjini, Bwana Paulo Kitosi akiwasilisha mada inayosema usimamizi wa masuala ya mazingira na jamii leo Juni 28,2024 katika mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa
milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ukiendelea leo Ijuma Juni
28,2024.
Mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa
milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ukiendelea leo Ijuma Juni
28,2024.
Mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa
milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ukiendelea leo Ijuma Juni
28,2024.
Mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa
milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ukiendelea leo Ijuma Juni
28,2024.
Mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ukiendelea leo Ijuma Juni 28,2024.
Post a Comment