Na Mapuli Kitina Misalaba
Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND
THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) ambaye ndiye muandaaji
wa Tamasha la utamaduni wa Msukuma ameshiriki
kupata baraka za wazee katika kijiji cha
Nhelegani kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.
Pamoja na mambo mengine MR. BLACK amepata wasaha wa
kunywa nao pombe ya kienyeji ya kisukuma na kucheza nao mchezo wa bao la kete
ikiwa ni kuenzi Tamaduni ya Msukuma katima michezo, asili na pombe asili.
Wazee wamemshukuru MR. BLACK kwa kuwa na uthubutu
katika kuchochea maendeleo kwa wakazi wa Nhelegani ambapo pia wamepongeza juhudi na ubora wa Tamasha hilo pia wameshauri mambo
mbalimbali huku wakiomba Tamasha hilo liwe endelevu.
Ikumbukwe kwamba muandaaji wa Tamasha la utamaduni
wa Msukuma ametokea katika familia ya
wauza pombe za kienyeji kapata elimu kupitia kipato cha uuzaji wa pombe za
kienyeji, "Jasiri haachi asili" nah ii ndiyo sababu kuwa inayopelekea kuendelea kuenzi mila na tamaduni za eneo hilo.
KUELEKEA TAMASHA LA UTAMADUNI WA MSUKUMA SHINYANGA, TAASISI YA THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION YAFANIKISHA MAREKEBISHO YA KUPAKA RANGI JENGO LA OFISI YA MAHAKAMA YA MWANZO MJINI SHINYANGA.
Tamasha la utamaduni wa Msukuma (SHINYANGA SUKUMA
FESTIVAL SEASON 3, ambalo limeandaliwa na THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED
AND THE TRUE LIVE FOUNDATION” Mwaka huu 2024 litafanyika kwa siku mbili kuanzia
Jumamosi Juni 29 hadi Jumapili Juni 30 katika viwanja vya shule ya msingi
Nhelegani kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga na kwamba hakuna kiingilio “SHINYANGA SUKUMA FESTIVAL SEASON 3,
LEJIGUKULU LYA NZENGO”.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika siku ya kufungua tamasha la utamaduni wa Msukuma
Jumamosi Juni 29,2024.
Naibu katibu mkuu wizara ya utamaduni, sanaa na
michezo Dkt. Suleiman Serera anatarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya kufunga
tamasha la utamaduni wa Msukuma Jumapili Juni 30,2024.
Katika tamasha hilo yatafanyika maonyesho ya
Biashara, sanaa, ngoma za asili, burudani pamoja na Nyama choma” ambapo kauli
mbiu ya tamasha la utamaduni wa Msukuma kwa Mwaka huu 2024 inasema “UTAMADUNI
WETU URITHI WETU, SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA MAENDELEO YA TAIFA”
Tamasha hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, taasisi binafasi, vyama, wadau pamoja na wananchi ambapo pia wageni kutoka ndani na nje ya Tanzania watakuwepo.
Post a Comment