Na Elisha Petro
Meneja
Mradi wa Shirika la Green Community Innitiative (GCI) Bwana Ngolelwa Enos
Masanja amewaomba wazazi na walezi katika jamii kuwa mabalozi wa kupiga vita mila na desturi
kandamizi zinazochochea ukatili kwa wanawake na watoto.
Bwana Ngolelwa amebainisha hayo wakati akitoa semina ya kupinga ukatili katika uwanja
wa shule ya msingi Lohumbo iliyopo kata ya Itwangi na kuwaomba wananchi wote
kuwa mabalozi wa kupinga ukatili kuanzia ngazi ya familia kwa kuibua na
kuripoti changamoto mbalimbali zinazochochea ukatili.
‘‘…hapa kata ya Itwangi tumepokea kesi nyingi sana
za ukatili wa kiuchumi wanaume wenzangu tunatumia rasilimali za familia ikiwemo
mazao,fedha na mali zingine kwa mambo yasiyo ya msingi ikiwemo kuhonga hayo
yote hayana faida ndani ya familia zetu tuache, pia tumepokea kesi za wazazi na
walezi kuwazuia watoto kwenda shule wengine wanawaruhusu lakini wakirudi kutoka
shuleni hawawapi chakula huo pia ni ukatili niwaombe tunapoona viashiria vya
ukatili tusiogope kuyaibua maovu na kuyafikisha kwa viongozi wetu wa serikali
ili kupinga ukatili katika familia na jamii yote’’
Kwa
upande wao viongozi wa serikali kata ya Itwangi wameahidi kuendelea
kushirikiana na mashirika mbalimbali yanayojitokeza kutoa elimu ya kupinga
ukatili ikiwemo shirkika la Green Community
Innitiative (GCI) na kuwaomba wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi inapotokea fursa ya kupata elimu hiyo.
‘‘… wazazi na walezi wenzangu niwaombe tuwajibikie
vema jukumu la malezi na makuzi kwa watoto wetu tuwapende,tuwajari,tuwasikilize
na kuwalinda na mambo yote ya ukatili yaliyomo katika familia na hata jamii
zetu pia tutambue umuhimu wa elimu jamoni tuwapeleke watoto shuleni huko
watafundishwa mabaya ya ukatili na namna ya kuyafikisha kwetu na tutawasaidia
kutimimiza ndoto zao’’ Amesema kaimu Afisa
maendeleo ya jamii kata ya Itwangi Bi. Fatuma Mrema
Kamuli
Sanyiwa Makomango ni Afisa Mtendaji wa kijiji cha Itwangi amewasisitiza
wananchi kuitumia vema elimu waliyoipata kwani elimu haina mwisho na inaendelea
kuishi.
‘‘ndugu zangu tusichoke kujifunza kila siku kwani
elimu haina mwisho na inaendelea kuishi kila kukicha leo GCI wamefika hapa
wametupa elimu ya kupinga ukatili niwaombe elimu hii tukaitumie katika familia
zetu mpka ngazi ya jamii na sisi viongozi wenu tuwahakikishie kuendelea
kushirikiana na haya mashirika kuja kutoa elimu’’
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza katika semina hiyo wamelipongeza shirika la Green
Community Innitiative (GCI) kwa elimu waliyoitoa na kuahidi kwenda kuifanyia
kazi elimu hiyo na kuwa mabalozi wa kupinga ukatili katika familia jamii na
kuliomba shirika hilo kuendelea kutoa elimu ili kutokomeza ukatili.
Sanjari
na hayo timu ya Majiji FC imefanikiwa kushinda goli 4 – 0 katika mchezo wa
ufunguzi wa semina hiyo na kutwaa kombe.
Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa Meneja Mradi wa Shirika la Green Community Innitiative (GCI) Bwn. Ngolelwa Enos Masanja amebainisha kuwa wataendelea kutoa elimu katika kata mbalimbali ikiwemo kata ya Nsalala kijiji cha Mwamkanga .
Post a Comment