Na Mapuli Kitina Misalaba
Watoto na vijana chini ya umri wa Miaka 17 kuendelea kunufaika na mradi wa “USAID Kizazi Hodari” unaotekelezwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika Mikoa tisa (9) Nchini kwa ufadhili wa shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa (USAID).
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mshiriki
anayesimamia matokeo na asasi zinazotekeleza mradi wa “USAID Kizazi Hodari” Kanda ya Kaskazini mashariki Bwana Aminiel
Alten Mongi kwenye kikao cha tathmini ya
utekelezaji wa mradi huo leo Juni 27,2024 Mkoani Shinyanga.
Amesema mradi huo pamoja na mambo mengine umelenga
kuboresha Afya, ustawi na ulinzi wa watoto walio katika mazingira hatarishi na vijana
chini ya Miaka 18 ili kutokomeza maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.
“Mradi
huu unafadhiliwa na shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani USAID ambao
ndio wafadhili wakuu wa mradi huu na mradi unatekelezwa na makao makuu ya
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mradi huu unatekelezwa katika
Mikoa tisa (9) ikiwa na jumla ya Halmashauri 41 Mikoa hiyo ni Tanga,
Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Singida, Dodoma, Mwanza, Geita pamoja na Mara”.
“Lengo
kuu la mradi huu ni kuboresha Afya, ustawi na ulinzi wa watoto waliokatika
mazingira hatarishi na vijana kuanzia umri wa Miaka 0 hadi 17 ili kufikia
malengo ya kidunia ya kupambana na virusi vya UKIMWI kwa maana wale wenye
maambukizi waweze kujua hali zao za maambukizi lakini pia wale ambao wamefahamu
hali zao za maambukizi waweze kuunganishwa na vituo vya tiba na mafunzo kwa
ajili ya kuanzishiwa dawa lakini pia wale ambao wameanzishiwa dawa kufika
kwenye vituo ili kufubaza maambukizi ya virusi vya UKIMWI”.
amesema Mongi
Mongi amesema makundi yanayofikiwa wakati wa utekelezaji
wa mradi huo ni pamoja na watoto walioathirika na viruri vya UKIMWI, watoto wa
wanawake walioko katika mazingira hatarishi pamoja na watoto walioathirika na
matukio ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia ambapo amesema kupitia mradi huo
watoto wanapata huduma mbalimbali zikiwemo za kiafya.
Ameeleza zaidi kuwa zipo afua mbalimbali ambazo
zinalenga kuwaimarisha kiuchumi walezi wa watoto pamoja na mabinti au wanawake
walio katika umri mdogo kwenye ngazi ya kaya huku akitaja shughuli zingine
zinazofanyika ambazo zinagusa sekta mbalimbali ikiwemo Afya na Elimu.
“Lakini
kuna maeneo ambayo tunayalenga katika utoaji wa huduma ikiwemo suala la Afya tunahakikisha
walengwa wanakuwa na Afya bora ambapo pia tunatoa huduma ya bima za Afya ili waweze kupata matibabu pale wanapokuwa
wagonjwa lakini pia kupewa elimu ya Afya ya uzazi na huduma zingine lakini pia
kuna huduma ya elimu tunahakikisha wanafunzi wanahudhuria shule na tunafuatilia
matokeo yao shuleni lakini pia tunawapa vifaa vya shule, pia kupitia mradi huu
tunawasaidia mfano kuwapa elimu ya biashara elimu ya fedha yaani kuweka na
kukopa pamoja na vifaa anzishi vya biashara ili waweze kuanzisha biashara ndogo
ndogo na hapa tunalenga kwenye suala la endelevu wa mradi lakini pia kuna nyanja
ya ulinzi na usalama ambapo tunahakikisha kuwa tunawalinda hata kwenye matukio ya
unyanyasaji na ukatili wa kijinsia tunawasaidia ili waweze kubaki kuwa salama”.
“Tulikuwa
na malengo ya kuwafikia wanufaika lakimoja na elfu 57, 110 lakini kufikia Mwezi
wa tatu ambayo ni tathmini ya nusu Mwaka tumeweza kuwafikia lakimoja 57 elfu 974
ambayo ni sawa na asilimia 105 lakini pia tulikuwa na malengo ya kuwafikia
wanufaika katika shughuli za kiuchumi ambapo tulilenga kuwafikia watu elfu
59,162 lakini kufikia Mwezi wa tatu katika kipindi cha nusu Mwaka tumewafikia
watu 62, 132”.amesema Mongi
Akizungumza mchumi mkuu idara ya Afya, lishe na
ustawi wa jamii kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI, Bwana Rashid Kitambulio amesema
serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa la KKKT katika kufikia malengo
yaliyokusudiwa huku akishukuru kwa mradi huo wa USAID kizazi hodari ambao
unaendelea kuwanufaisha wahanga hasa wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
“Tunashirikiana
na Kanisa la KKKT kuhakikisha kwamba shughuli ambazo zimepangwa kufanyika zinafanikiwa
na ushiriki wetu mkubwa upo katika eneo la usimamizi ambapo tunahakikisha
kwambwa wale walengwa wanapata zile huduma zilizokusudiwa lakini eneo lingine
tunashirikiana katika kuzipitia taarifa za utekelezaji wa mradi huu, tukiangalia
moja ya mafanikio ni kwamba hizi jamii ambazi zilikuwa zimesahaulika kwa sasa
hivi tumeweza kuzibaini kupitia mradi wa USAID Kizazi Hodari na tunashukuru walengwa wanaendelea kunufaika”.amesema
Kitambulio
Kwa upande wake mganga mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt.
Zabron Masatu amesema mradi wa USAID kizazi hodari umekuwa na manufaa makubwa
hasa katika sekta ya Afya ambapo pamoja na mambo mengine baadhi ya familia
wamepatiwa ufadhili wa kadi za bima ya Afya ICHF ambapo amesema kandi hizo
zimekuwa zikiwasaidia katika kupata matibabu watoto na familia kwa ujumla.
Naye mratibu wa Mikoa na Halmashauri kutoka tume ya
kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) amepongeza kwa mradi huo kuendelea
kuwatambua na kuwawezesha kupata huduma zinazistahili waathirika wa virusi vya
UKIMWI ambapo ameshauri mradi huo wa ‘USAID Kizazi Hodari’ kuwa endelevu ili
kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mradi wa ‘USAID Kizazi Hodari’ limeitisha mkutano wa wadau wanaoshiriki katika utekelezaji wa mradi huo wakiwemo wawakilishi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundu maalum, TACAIDS, kamati ya usimamizi wa Afya ngazi ya Mikoa na Halmashauri, wadau wanaosimamia afua za tiba na mafunzo katika Mikoa husika ili kupitia na kutathimini utekelezaji wa shughuli za mradi na kuweka mipango endelevu ya mradi huo.
Mratibu wa kudhibiti UKIMWI Mkoa wa Shinyanga akizungumza leo Juni 27,2024.
Mratibu wa Mikoa na Halmashauri kutoka tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Amina Masood akizungumza leo Juni 27,2024.
Mkutano wa wadau wanaoshiriki katika utekelezaji wa mradi huo wakiwemo wawakilishi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundu maalum, TACAIDS, kamati ya usimamizi wa Afya ngazi ya Mikoa na Halmashauri, wadau wanaosimamia afua za tiba na mafunzo katika Mikoa husika ukiendelea leo Alhamis Juni 27,2024.

Mkutano wa wadau wanaoshiriki katika utekelezaji wa mradi wa ‘USAID Kizazi Hodari’ ukiendelea katika ukumbi wa mikutano Vigimark Hotel Manispaa ya Shinyanga Juni 27,2024.

Post a Comment