Na Amina Mbwambo, Kahama
Wakazi wa Wilaya ya Kahama
Mkoa wa Shinyanga washauriwa kutokununua madini mtaani bali waende
wakauziane na wateja wao kwenye soko la madini ili kuepuka utapeli
wa madini ya dhahabu ulioanza kushamiri katika mkoa wa kimadini Kahama.
Wito huo umetolewa
Juni 28, 2024 na Afisa Madini
Mkazi Mkoa wa kimadini Kahama Mhadisi Joseph Kumbulu, baada ya ofisi yake kuweka mtego
uliofanikisha kumkamata mwanaume mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa mkazi wa Geita aliyekuwa
akifanya vitendo vya kuwatapeli wananchi wilayani Kahama huku akijitambulisha
kama Afisa madini.
Kwa mujibu wa Mhandisi Kumburu, ameeleza kuwa mtu huyo amekuwa
akifanya vitendi hivyo kwa kusaga kufuli la kufungia mageti na milango na kisha
kuiweka kwenye vifungashio maalum huku akidanganya kuwa ni dhahabu.
“Kwa
muda wa miezi miwili sasa katika Mkoa wa kimadini kahama kumetokea wimbi la
utapeli kwa baadhi ya watu kujiita maafisa madini wamekuwa wakitumia makufuli
yenye rangi ya dhahabu wanayapondaponda na kuweka kwenye chupa wanatapeli watu,
kuna watu walikuja kulalamika kuna watu wamewatapeli ambao wanajiita maafisa
madini hivyo tulifanya mtego na tukamkamata”,amesema Kumbulu .
Mwanaume huyo mwenye umri wa Miaka 58 ameeleza jinsi alivyokutwa na madini
hayo feki ya dhahabu katika kituo kidogo cha mabasi kilichopo Majengo Kahama,
na alipigwa sana na watu wanaojiita polisi jamii manusura kufa, analishukuru
jeshi la polisi kufika katika eneo hilo na kumuokoa kwa watu wenye hasira kali
akiwa hoi.
Ameishukuru serikali kupitia wizara ya madini , mkoa wa kimadini Kahama kwa kumsamehe baada ya kukiri makosa yake na kumpa elimu, pia amewatahadharisha wananchi wenye tabia ya utapeli waache maana utapeli ni kifo.
Alipotafutwa kuzungumzia hali hiyo, kaimu kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Kennedy Mgani alisema kuwa bado halijafika mezani kwake na kuahidi kuwa analifuatilia na kwamba atalitolea ufafanuzi baadae litakapokamilika.
Afisa Madini Mkazi Mkoa wa kimadini Kahama Mhadisi Joseph Kumbulu akizungumza na Misalaba Media.TAZAMA VIDEO
Post a Comment