" ANDENGENYE APONGEZA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO KIGOMA

ANDENGENYE APONGEZA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO KIGOMA

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma    Thobias Andengenye amemshukuru Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kukipa kilimo msukumo  na kuwezesha kutengwa bajeti kubwa  kupitia Wizara ya Kilimo hivyo kufanya mageuzi makubwa kwenya Sekta ya Kilimo kwa lengo la kuwawezesha wakulima kufanya kilimo biashara chenye Tija.

 

Andengenye ametoa kauli hiyo mji Kigoma akikabidhi vitendea kazi kwa maafisa Ugani wa mkoa wa Kigoma ili kuwezesha  nyenzo hizo kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na Serikali katika kukifanya kilimo kuwa na tija kubwa.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa wakati huu ambao serikali imeutangaza mkoa Kigoma kuwa mkoa wa kimkakati katika masuala ya uchumi na biashara  sekta hiyo ina  umuhimu mkubwa katika kutekeleza mpango huo kwani sekta hiyo inagusa shughuli na Maisha ya kila siku ya wananchi wote wa mkoa Kigoma.

 


Aliema kuwa asilimia 70 ya wakazi wa mkoa Kigoma hutegemea shughuli za kilimo kama chanzo chao kikuu cha uchumi kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku hivyo ametaka nyenzo hizo zilizokabidhi zitumike katika kutekeleza mikakati ya kuimarisha shughuli za kilimo na kuwafikia wadau wote wa kilimo  kwa wakati

 

Aidha Mhe. Andengenye amezikumbusha halmashauri kutekeleza maagizo ya Waziri wa Kilimo , Hussein Bashe ikiwemo halmashauri ya Kigoma Ujiji ku kutenga eneo ili wizara hiyo iweze kutekeleza mradi wa ujenzi wa Kituo cha kuratibu shughuli za umwagiliaji nchini.

Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post