Na Mapuli Kitina Misalaba
Mashirika
yasiyo ya kiserikali (NGOs) Wilayani Shinyanga yameomba ushirikiano zaidi na
serikali ili kufanikisha utawala bora na maendeleo endelevu.
Hayo yamesemwa leo Agosti 21, 2024, na Naibu
Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la SHDEPHA, Bi. Shekha Nassoro, katika risala
ya mashirika hayo kwenye Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO)
lililofanyika katika ukumbi wa Rafiki SDO Mjini Shinyanga.
Amesema mashirika yasiyo ya kiserikali yanachangia
kwa kiasi kikubwa katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, afya, haki za
binadamu, na mazingira, huku yakiwa mstari wa mbele katika kulinda haki za binadamu yakiwemo makundi ya wanawake na watoto.
Bi. Shekha ameongeza kuwa mashirika haya yamekuwa kiungo
muhimu cha maendeleo, lakini yanakutana na changamoto mbalimbali zinazokwamisha
utekelezaji wa miradi yao, ikiwemo uelewa mdogo wa jamii kuhusu majukumu yao na
changamoto za kisheria na kiutawala.
"Mashirika
yasiyo ya kiserikali yamekuwa kiungo muhimu katika kutoa sauti kwa makundi
yaliyo pembezoni na kuwa mstari wa mbele katika kulinda haki za binadamu,"
alisema.
“Changamoto
hizi, pamoja na ushirikiano hafifu kutoka kwa baadhi ya viongozi wa serikali
ngazi za vijiji na vitongoji, zinahitaji kushughulikiwa ili tuweze kufanikisha
malengo yetu ya kuleta maendeleo na kuimarisha utawala bora,”
amesema Bi. Shekha.
Baadhi ya viongozi wa mashirika mbalimbali waliotoa
maoni yao katika jukwaa hilo, wameeleza kuwa bado kuna changamoto kubwa ya ndoa
za utotoni na ukatili wa kijinsia, ambapo wahanga wanakosa mazingira salama ya
kulinda haki zao, hasa wakati wa kesi zao.
Wameiomba serikali kuweka mazingira bora zaidi ya
ulinzi, ikiwemo kuanzisha nyumba salama kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.
"Wahanga
wa vitendo hivi wanakosa mazingira salama ya kuwalinda, ikiwemo nyumba salama
wakati wa kesi zao,".
Pia walitoa ombi kwa serikali kuweka mfumo maalum wa
kusaidia mashirika madogo yanayochipukia ili yaweze kushirikiana na mashirika
makubwa yanapotekeleza miradi yao.
“Kuna
mashirika madogo yanayojitahidi kutoa huduma katika jamii, lakini yanakabiliwa
na changamoto za kifedha, tunashauri kuwe na mfumo maalum wa ushirikiano kati
ya mashirika makubwa na madogo ili kuhakikisha kuna mwendelezo wa miradi hata
pale mashirika makubwa yanapoondoka,” amesema mmoja wa
viongozi hao.
Vilevile, viongozi hao walilalamikia ucheleweshaji
wa takwimu muhimu zinazohusiana na matukio ya ukatili wa kijinsia.
Walipendekeza kuboreshwa kwa mfumo wa upatikanaji wa takwimu hizo ili
kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.
"Tunaomba mfumo wa upatikanaji wa takwimu
hizi uboreshwe ili mashirika yawe na uwezo wa kupata takwimu hizi moja kwa moja
kutoka kwa viongozi wa MTAKUWWA,".
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro,
ameyapongeza mashirika hayo kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuahidi ushirikiano
wa karibu kati ya serikali na NGOs ili kuimarisha utawala bora na maendeleo
katika Wilaya ya Shinyanga.
Amesema
serikali itaendelea kushughulikia changamoto zinazokwamisha mashirika hayo
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, huku akitoa wito kwa watumishi wa ngazi za
chini kushirikiana na mashirika hayo kwa maslahi ya wananchi.
Kwa upande wake, Kiongozi wa NACONGO Wilaya ya
Shinyanga, Bwana Lucas Daud, amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa ushirikiano wake na
kuahidi kuwa mashirika hayo yataendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na
kufuata sheria na taratibu za nchi.
Kaulimbiu ya jukwaa hilo inasema "MASHIRIKA
YASIYO YA KISERIKALI NI WADAU MUHIMU, WASHIRIKISHWE KUIMARISHA UTAWALA
BORA."
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza kwenye jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali Wilaya ya Shinyanga Agosti 21,2024.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza kwenye jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali Wilaya ya Shinyanga Agosti 21,2024.
Naibu Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la SHDEPHA, Bi. Shekha Nassoro, akisoma risala ya mashirika hayo kwenye Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) lililofanyika katika ukumbi wa Rafiki SDO Mjini Shinyanga Agosti 21,2024.
Kiongozi wa NACONGO Wilaya ya Shinyanga, Bwana Lucas Daud, akizungumza kwenye Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) ambalolimefanyika katika ukumbi wa Rafiki SDO Mjini Shinyanga Agosti 21,2024.
Kiongozi wa NACONGO Wilaya ya Shinyanga, Bwana Lucas
Daud, akizungumza kwenye Jukwaa la
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) ambalolimefanyika katika ukumbi wa
Rafiki SDO Mjini Shinyanga Agosti 21,2024.

Jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali Wilaya ya
Shinyanga likiendelea katika ukumbi wa mikutano Rafiki SDO mjini Shinyanga
Agosti 21,2024.
Meneja miradi wa hirika la Companion of Women and Children Empowerment (COWOCE)
, Nyakabhi Zoma, akizungumza kwenye jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali Wilaya ya Shinyanga Agosti 21,2024.Mwenyekiti wa kamati ya huduma wa msaada wa kisheria Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni kaimu mkurugenzi wa Shirika la msaada wa kisheria la Paralegal Aid Centre Shinyanga (PACESH) Bwana John Shija akizungumza kwenye jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali Wilaya ya Shinyanga Agosti 21,2024.
Mwenyekiti wa kamati ya huduma wa msaada wa kisheria Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni kaimu mkurugenzi wa Shirika la msaada wa kisheria la Paralegal Aid Centre Shinyanga (PACESH) Bwana John Shija akizungumza kwenye jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali Wilaya ya Shinyanga Agosti 21,2024.
Naibu Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la SHDEPHA,
Bi. Shekha Nassoro.
jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali Wilaya ya Shinyanga likiendelea katika ukumbi wa mikutano Rafiki SDO mjini Shinyanga Agosti 21,2024.

Post a Comment