Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwanaume mmoja aitwaye Charles Kastory Kashinje,
mwenye umri wa miaka 24 na mkazi wa kijiji cha Idodoma, kata ya Samuye,
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, amekutwa ameuawa kwa kukatwa sehemu
mbalimbali za mwili wake kando ya barabara.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumatatu,
Septemba 9, 2024.
Misalaba Media imefanya mahojiano na Mwenyekiti wa
kijiji cha Idodoma, Bwana Masesa Izengo Chaba ambaye ameeleza jinsi alivyopokea
taarifa hizo.
“Nilipewa taarifa saa mbili asubuhi kwamba kijana
mmoja ameuawa kwa kukatwa mapanga na kuchinjwa, marehemu ni dereva wa bodaboda
na alikuwa anaishi na baba yake, akiwa na mke na watoto wawili wa kike, mwili
wake ulikutwa jirani na mto wa Idodoma, umelazwa kwenye pikipiki yake baadaye polisi walikuja wakauona huo mwili badaye
wakaruhusu kuendelea na taratibu za mazishi kwahiyo tayari jioni ya leo
amezikwa”.amesema Mwenyekiti Chaba
Diwani wa viti maalum kata ya Samuye, Mhe. Leticia
Masalu naye ameongelea tukio hilo.
“Na
mimi nilipigiwa tu simu asubuhi nikaambiwa kuna mtu ameuawa yaani amechinjwa wamemkuta
tu eneo la Idodoma lakini kuna poli eneo hilo nyumba zipo mbali, kweli nimefika
kwenye eneo la tukio nikaona, niwaombe tu wananchi tuwe makini maana hili
limekuwa ni janga kubwa sana tuzingatie usalama wetu hasa inapofika usiku tusitembee
peke”.amesema Mhe. Leticia
Misalaba Media inaendelea kufuatilia taarifa zaidi
kutoka kwa mamlaka husika, ikiwemo Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ili
kupata maelezo ya kina kuhusu tukio hilo na hatua zinazochukuliwa.
0 Comments