Na Mapuli Kitina Misalaba
Michuano ya Krismas CUP iliyokuwa ikifanyika kwa takribani mwezi mmoja sasa inafikia kilele chake leo, Desemba 19, 2024, kwa mechi ya fainali kati ya Salawe Stars na Beya FC.
Michuano hii imeandaliwa na Makamba Mussa Lameck kwa lengo la kuhamasisha michezo na mshikamano katika jamii.
Akizungumza na MisalabaMedia, Makamba Mussa Lameck amewahimiza wananchi wa Salawe na maeneo ya jirani kufika kwa wingi kushuhudia fainali hii ya kusisimua itakayofanyika kwenye uwanja wa Mhangu kata ya Salawe kuanzia saa 09:30 jioni.
Fainali ya leo inatarajiwa kuwa na ushindani mkali, huku Salawe Stars na Beya FC zikijizatiti kuibuka na ushindi.
Makamba amesema mshindi wa kwanza atakabidhiwa kombe na kitita cha fedha, huku nafasi ya pili naya tatu nao watapata zawadi ya fedha ambapo wachezaji walioonyesha umahiri watapewa zawadi maalum.
Michuano ya Krismas CUP imekuwa kivutio kikubwa kwa jamii, ambapo timu kutoka maeneo mbalimbali zimepata nafasi ya kushindana na kubadilishana uzoefu wa michezo.
MISALABA MEDIA itakuwa na ripoti ya kina kuhusu fainali hii, ikikuletea matukio yote muhimu yanayojiri kwenye uwanja wa Mhangu.
Makamba Mussa Lameck.
Makamba Mussa Lameck
Post a Comment