Na Elisha Petro, Misalaba Media
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amewashukuru Wananchi wa Wilaya ya Shinyanga Mjini kwa kushiriki vyema kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji huku akiwaomba wazidi kuwaamini na kuwapa ushirikiano Viongozi wao kwa kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu.
Bwana Mlolwa ameyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga ulioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wenye lengo la kuwashukulu wananchi kwa kuendelea kukiamini chama hicho na kuwataka viongozi waliochaguliwa kuwa waadilifu,wachapakazi na kutenda haki pindi wanapotoa huduma kwa wananchi bila kujali tofauti za vyama .
"Bila kujali rangi kabila lako, Chama chako viongozi hawa mliowachagua watawahudumia niwaombe na sana viongozi msiende kufanya kazi kwa kuwabagua Watanzania wa Manispaa ya Shinyanga muende muwapokee uwe uligombea naye au hujagombea naye toa huduma maelekezo ya Chama cha Mapinduzi ni kutoa huduma kwa Watanzania"
Katika hatua nyengine Mlolwa amevipongeza vyama vyote vya upinzani kwa kushiriki na kutoa upinzani mkubwa katika uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa uliopita kwani ni msingi bora wa Demokrasia nchini.
"Tutakuwa wachoyo wa fadhira Chama cha Mapinduzi tusipowashukuru vyama vingine rafiki wakiwemo CHADEMA na wote walioshiriki tunawashukuru sana kwa kushiriki uchaguzi wa Amani, wasingekuwepo tungetangazwaje tumeshinda lazima wawepo kwa hiyo nawashukuru sana salamu hizi muwafikishie na kama wapo naamini wananisikia tunawashukuru waendelea kushiriki chaguzi zinapokuja tushiriki kwa pamoja Mama yetu Daktari Samia Suluhu Hassan amepanua wigo wa Demokrasia"
Awali Katibu wa Siasa,Uenezi na Mafunzo Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Richard masele amewapongeza wananchi walioshiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kukiwezesha chama hicho kupata ushindi kwa asilimia kubwa ukilinganisha na vyama vya upinzani.
"katika Mkoa mzima wa Shinyanga tunavyo Vijiji 506 lakini Vijiji 504 vimekwenda kwa Chama cha Mapinduzi ushindi wa asilimia 99.6 lakini hiyo haitoshi tunavyo Vitongoji 2702 katika Mkoa wetu wa Shinyanga katika Vitongoji hivyo 2666 vimekwenda Chama cha Mapinduzi ushindi wa asilimia 99 kwa hiyo ndiyo maana mwenyekiti hii leo amekuja kuwashukuru na kusema nanyi"
Baada ya Mkutano wa hadhara uliofanyika Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mabala Mlolwa, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Bwana Anold Makombe,Wenyeviti wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji wamekaa kikao katika ukumbi wa mikutano Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom) chenye lengo la kuwakumbusha majukumu ,kuwatia moyo Wenyeviti wote waliochaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumzakwenyemkutanowahadhara leo Desemba 14, 2024.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo Desemba 14, 2024.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Richard Raphael Masele akizungumza kwenyemkutano wa hadhara leo Desemba 14, 2024..
Katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Richard Raphael Masele akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Anord Makombe akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo Desemba 14, 2024.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Anord Makombe akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Anord Makombe akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambullah akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara leo Desemba 14, 2024.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambullah akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara leo Desemba 14, 2024.
Burudani ikiendelea.
Mkutano wa hadhara ukiendelea.Mkutano wa hadhara ukiendelea.
Mkutano wa hadhara ukiendelea.Mkutano wa ndani ikiendelea leo Desemba 14, 2024.
Mkutano wa ndani ikiendelea leo Desemba 14, 2024.



































Post a Comment