Msimamizi wa Ligi ya Krismas Cup,
Mwalimu Emmanuel Enock Kijida, ametangaza mabadiliko ya ratiba ya mechi za
Fainali kufuatia tukio la msiba uliowakumba Beya FC.
MSHINDI WA TATU
- Tarehe:
16 Desemba 2024 (Jumatatu)
- Muda:
Saa 10:00 jioni
- Mechi:
Kano FC vs Mwasenge FC
- Uwanja wa Mhangu
FAINALI
- Tarehe:
18 Desemba 2024 (Jumatano)
- Muda:
Saa 10:00 jioni
- Mechi:
Beya FC vs Salawe Stars
- Uwanja wa Mhangu
Kwa mujibu wa Mwalimu Kijida, mabadiliko haya yamesababishwa na msiba wa bibi wa wachezaji na viongozi zaidi ya sita wa Beya FC, ambapo mazishi yatafanyika Jumanne, tarehe 17 Desemba 2024.Mwandaaji na mdhamini wa ligi hiyo Bwana Makamba Mussa Lameck kupitia kampuni yake ya MCL, ametoa pole kwa familia ya Beya FC kufuatia msiba wa bibi wa wachezaji na viongozi zaidi ya sita wa timu hiyo.Mashabiki wote wanahimizwa kuendelea kuonyesha mshikamano na kusapoti timu zao huku wakizingatia ratiba mpya.
Makamba Mussa Lameck.
Post a Comment