" TAMASHA LA KWANZA LA KIHISTORIA NA UTAMADUNI MJI MKONGWE LAFANA SANA.

TAMASHA LA KWANZA LA KIHISTORIA NA UTAMADUNI MJI MKONGWE LAFANA SANA.

Wakazi wa Mkoa wa Kigoma wameaswa Kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo mkoani humo ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Gombe ambayo ina wanyama aina ya sokwe mtu pamoja na maporomoko mazuri ya maji.

Wito huo umetolewa na Sheikh Hassan Kabeke wakati wa Tamasha la kwanza la kihistoria na Utamaduni wa Mji Mkongwe wa Kigoma ujiji lililolenga 
kutangaza mji huo mkongwe pamoja na vivutio kadhaa vya utalii vilivyopo mkoani Kigoma

Sheikh Kabeke ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tamasha hilo amesema kuwa ni Jukumu la kila mwana Kigoma wakiwemo wa Ujiji,Kasulu,Kibondo,Kakonko,,Buhigwe,Ilagala,Mwamgongo,Mwanga,Bangwe,Gundu,Mwandiga,Kibirizi kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo kwenye mji huo pamoja na Mkoa Kigoma kwa Ujumla. 

" Mji wa Kigoma Ujiji una zaidi ya miaka 300 na Majengo ya ibada na Misikiti yenye zaidi ya karne tano likiwemo Kanisa lenye umri wa miaka Mia Moja sanjari na visima vilivyo chimbwa wakati wa Utawala wa Waingereza"alisema Sheikh Kabeke kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wanatamasha hilo lililofana sana na kusisitiza umuhimu wa wana Kigoma kuupenda na kuuenzi mji huo. 

Shekh Hassan Kabeke amesema kuwa wakati wa Tamasha hilo wananchi wamepata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii 

Aidha amewakumbusha wana Kigoma kujenga tabia ya kurudi nyumbani kwa kila mwaka kwa ajili ya kuwaona wazazi,ndugu na jamaa.

Sheikh Kabeke pia ameipongeza Serikali kwa kuufungua Mkoa Kigoma ikiwemo kuanza kwa ujenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,ujenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kituo cha Kigoma,Bonde la Lwiche kujengwa kwa matumizi ya umwagiliaji na Barabara ya Kibondo na Uvinza ambazo zitakamilika hivi karibuni kukamilika kwa kiwango cha lami.

Shekh Hassan Kabeke amesema Tamasha hilo limempongeza kwa dhati Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoka Ikulu na kwenda kuigiza Filamu ya ROYAL TOUR ikiwa ni kutangaza vivutio vya utalii nchini ambapo katika kumuunga mkono wameamua kuutangaza mji wa kale wa Ujiji wenye Mambo mengi ya kuvutia na ambao umekuwepo kabla ya ujio wa Dkt.Livingstone 1871.

Mji wa Ujiji una makabila mbalimbali ikiwemo Wakusu,Waluba,Wagoma,Wanya,Karamba,Waha,Wabwari,Wabembe,Waororo,Wahombo,Watongwe pamoja na Wamasanze ambayo yameaswa kutokuogopa kujinasibu kwa kabila zao  huku wakiaswa kuendelea kutunza amani na utulivu nchini na kusimama kwa pamoja kwa umoja bila kutazamana kwa uislamu na ukiristo kama viongozi wa madhehebu mbalimbali walivyo wamoja. 

Kwenye kilele cha Tamasha hilo,Tuzo mbalimbali zimetolewa kwa baadhi ya watu waliowahi kutoa michango mbalimbali katika Mkoa na Nchi akiwemo Shekh Kaluta,Amri Abeid ambaye kwa mwaka huu anatimiza miaka 100 toka kuzaliwa kwake  huku akiwa mwafrika wa kwanza kuwa Waziri wa pili wa sheria,Waziri wa Utamaduni,Abeid aliyezaliwa mwaka 1924 na alifariki Mwaka 1964 akiwa na umri wa miaka 40 hivyo kwa mwaka huu ametimiza miaka 100.




 




Post a Comment

Previous Post Next Post