Na Belnardo Costantine, Misalaba Media
Walinda amani wa "SAMIDRC" waliotumwa chini ya Mwamvuli wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) waliokua wakilinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wameanza kuondoka, kupitia Rwanda mnamo Aprili kulindi nchini kwao.
Kikosi cha SADC, kinachojumuisha Wanajeshi kutoka Afrika Kusini, Tanzania na Malawi, kilifanya mchakato wa awali kwa uhakiki rasmi hati katika kivuko kikuu cha mpaka kati ya Rwanda na DRC kisha kuanza zoezi la kuondoka nchin DRC leo tarehe 29/4/2024 wao pamoja na vifaa vyao vya kijeshi.
Hatahivyo idadi kamili ya Wanajeshi waliohusika na zoezi hilo haijawekwa wazi kutokana na ombi la SADC.
Taarifa zinasema kundi hili la awali kuondoka ililenga kurudisha vifaa vya kijeshi sambamba na kikosi kidogo cha askari, huku makundi makubwa yakitarajiwa kufuata.
Wanajeshi hao wanasafiri kwa njia ya Rubavu-Kigali-Rusumo kuelekea Wilaya ya Chato kaskazini-magharibi mwa Tanzania.
Post a Comment