" CHAMA CHA WAGANGA WA TIBA ASILI (TAMESO) CHAWAFUNZA WAGANGA

CHAMA CHA WAGANGA WA TIBA ASILI (TAMESO) CHAWAFUNZA WAGANGA



Chama cha Waganga wa Tiba Asili chini ya Katibu Mkuu Lukas Mlipu kimetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kutoa Elimu ya kuwasaidia katika Shughuli zao mafunzo ayo yanalenga kuwasaidia katika Majukumu Yao 

Akizungumza Lucas Mlipu Tarehe 28/6/2025 Dodoma Amesema Inapokalibia Miezi ya Uchaguzi tunaona Mengi yanatokea Ikiwemo watu wengi kupoteza Viungo vyao na kupoteza Maisha Hasa  watu wenye hualbino hivyo niwaombe Waganga nchi nzima kutojiusisha na Ramli za Viungo vya watu namna hiyo Inaweza  kuvunja Amani kwenye nchi yetu.

Lucas amewataka Waganga waendelee kumwamini Mungu wanapokuwa wanatoa Tiba zao lkn pia ameishuru selikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyojali Sekta Iyooo 

Alisema Sisi Kama umoja wa Waganga Tunaunga Mkono  juhudi za Mhe,Rais kuelekea  Uchaguzi Mkuu  ambao ni October mwaka huu mafunzo hayo yana kauli mbiu”Maendeleo ya Tiba Asili ni Jukumu letu sote.

Post a Comment

Previous Post Next Post