Na Mwandishi Wetu, Manyoni
Wananchi wa Jimbo la Manyoni wameendelea kuonyesha imani kubwa kwa Kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sultan Nassor Sultan, baada ya kuchukua rasmi fomu ya kugombea Ubunge kupitia chama hicho.
Sultan Nassor Sultan, anayefahamika kwa hoja zake zenye mashiko, uongozi wenye maono na moyo wa kushirikiana na jamii, amesisitiza kuwa safari yake ni kuhakikisha wananchi wa Manyoni wanapata uwakilishi thabiti, unaogusa maisha yao moja kwa moja.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu katika Ofisi za CCM, Sultan alisema: "Nimekubali wito wa wananchi wa Manyoni. Dhamira yangu ni kusimama kwa ajili ya kuboresha afya, kuinua elimu, kuimarisha miundombinu na kuweka mazingira bora ya ajira na ujasiriamali kwa vijana wetu. Tumefika wakati wa Manyoni kusonga mbele kwa umoja na mshikamano.”
Kauli hiyo imepokewa kwa shangwe na wananchi na wafuasi wake, ambao wanaamini Sultan ndiye chaguo sahihi kupeleka Manyoni katika hatua mpya ya maendeleo endelevu. Wengi wamesema wana matumaini makubwa kwamba atakuwa daraja la kuunganisha makundi yote – vijana, wanawake, wazee na wajasiriamali – ili kuharakisha mafanikio ya kiuchumi na kijamii jimboni humo.
Viongozi wa CCM katika jimbo hilo wamemwelezea Sultan kama kiongozi mwenye msimamo wa haki, anayejua kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi kwa vitendo.
Post a Comment