" NICKSON GEORGE AWATAKA VIJANA WAACHE KUJIBWETEKA, WATUMIE VIPAJI KAMA FURSA YA KIPATO

NICKSON GEORGE AWATAKA VIJANA WAACHE KUJIBWETEKA, WATUMIE VIPAJI KAMA FURSA YA KIPATO


Kiongozi wa ubunifu na mikakati na msimamizi wa chapa kampuni ya jambo Group NICKSON GEORGE akizungumza

Na Suzy Butondo, Shinyanga 

Kiongozi wa ubunifu na mikakati na msimamizi wa chapa kampuni ya jambo Group NICKSON GEORGE amewataka vijana kutumia majukwaa mbalimbali kuonesha vipaji vyao ili waweze kuvitumia na kujipatia kipato, wasikae na kujibweteka wakitegemea kuajiliwa   na kushindwa kufikia ndoto zao na wengine kujiunga na makundi maovu.

George ameyasema wakati wa kampeni maalum ya mimi mwamba iliyolenga kuibuwa vipaji, mbalimbali kwa vijana, ambapo amewaomba wazazi kuacha kuwaficha watoto wao ili wafikie ndoto zao.

"Kampuni ya jambo mara nyingi imekuwa ikiitisha matamasha ya kuibua vipaji mbalimbali vya watoto, na leo imezindua kampeni maalumu ya mimi Mwamba ambayo imelenga kuibua vipaji malimbali  vya vijana   niwaombe sana wazazi muwaruhu vijana wawe wanajitokeza kwenye matamasha haya "amesema George.

Aidha baadhi ya vijana waliojitokeza kuonesha vipaji vyao akiwemo Idd Sima,msanii wa muziki  Yona Msi msanii wa nyimbo,  Chita Boy mbunifu wa mitindo  na Elias Nyanda  wameishukuru kampuni ya jambo group kwa hatua ambayo imewezesha kuwaibuwa vijana wengi ambao vipaji vyao vilikuwa vimejificha.

Katika tamasha hilo vijana mbalimali walionyesha vipaji vyao ambapo washindi walipatiwa zawadi mbalimbali, walionyesha vipaji mbalimbali  ikiwa ni pamoja na kuimba, kucheza, kupiga danadana, pamoja na kushiriki mashindano ya kula ugali,mikate, na kuvuta kamba.



 



Post a Comment

Previous Post Next Post