" TAKUKURU YATAKIWA KUONGEZA JITIHADA KATIKA MAPAMBANO YA RUSHWA

TAKUKURU YATAKIWA KUONGEZA JITIHADA KATIKA MAPAMBANO YA RUSHWA

 
 
 
Na Lucas Raphael,Tabora

Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora  Deuc Sangu ,ameitaka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) kuongeza jitihada katika mapambano ya rushwa za aina zote bila kujali kubwa au ndogo.
 
Lengo likiwa ni  kuwaondolea malalamiko kero wananchi  hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi octoba mwaka huu .
 
Alitoa maagizo hayo  wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la Ofisi ya TAKUKURU wilaya ya nzega mkoani Tabora, lililogharimu kiasi cha shilingi milioni 314.2.
 
Alibainisha kwamba lengo  muhimu la Taasisi hiyo nikuvishughulikia vitendo vyote vya rushwa ambavyo vinasababisha wananchi kushindwa kupata haki zao kutokana na wachache kutokuwa waaminifu au kutumia vyeo vyao,ukubwa wao na umaarufu wao kukandamiza haki za wengine.
 
Alisema kwamba serikali ya awamu ya sita haitaweza kuvumilia vitendo hivyo bali ni kupambana navyo na kuvikomesha kabisa.
 
Saungu alifafanua lkamba Katika kuhakikisha vitendo vya rushwa vinapungua na hata kumaliza kabisa hapa nchini ni lazima kila mwananchi kushiriia katika kutokomeza vitendo vyote vinavyoohashiria rushwa vinafichuliwa .
 
 
Awali akitoa taarifa juu ya ujenzi wa jengo hilo, mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU ,Crispin Chalamila Alisema kwamba Taasisis ihiyo imepatiwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo yao wenyewe kuliko kuendelea kupanga majengo ya watu binafsi .
 
Alisema kwamba tayari wamejenga majengo katika mikoa 5 na wilaya 19 katika kipindi hiki cha mwaka 2025 na kusisitiza kumaliza kwa jengo hilo kutaongeza ufanisi katika utendaji wa taasisi hiyo mkoani tabora.
Mwisho



 

Post a Comment

Previous Post Next Post