" Yanga Wapo Kambini, Huenda Hii Hatuchezi ni Danganya Toto…

Yanga Wapo Kambini, Huenda Hii Hatuchezi ni Danganya Toto…

Yanga SC wanaimba hawachezi. Wimbo wao umekwenda mbali kidogo na matumaini ya Mchezo wa Derby yameanza kuwa madogo. Nini wanachopaswa kufanya Simba SC katika kipindi hiki cha Hatuchezi ng’oo?

Wajiandae na mechi, hii hatuchezi ng’oo isiwaingie wao. Kama timu wajiandae kikamilifu kwa ajili ya mchezo huo bila kutazama nini kinazungumzwa katika mitandao. Yanga SC wako kambini. Wanajiandaa na michezo iliyobakia. Kuna baadhi ya wachezaji wao hawakwenda na Stars kule Polokwane Afrika Kusini. Mudathir Yahya na Clement Mzize. Wamebaki zao Avic Town kufanya mazoezi. Wakubwa hii inatufikirisha kitu.

Simba SC wajiandae na mechi. Lolote linaweza kutokea katika muda wowote, hii hatuchezi isiwaingie wao, ibakie nje kwa mashabiki na wanachama wao, lakini ndani ya uwanja Mnyama ajiandae kiwasasawa.


Post a Comment

Previous Post Next Post