" ABDALLAH MAULID AOMBA RIDHAA YA CCM KUGOMBEA UDIWANI KATA YA MASEKELO

ABDALLAH MAULID AOMBA RIDHAA YA CCM KUGOMBEA UDIWANI KATA YA MASEKELO

Na Mapuli Kitina Misalaba

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Maulid Abdallah, ametangaza nia ya kuwania nafasi ya Udiwani katika Kata ya Masekelo, Manispaa ya Shinyanga, kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Abdallah Maulid tayari amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake ili kumpitisha kuwa mgombea rasmi wa nafasi hiyo, akilenga kuendeleza jitihada za kuwaletea maendeleo wananchi wa Masekelo.

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu hiyo katika ofisi ya CCM Kata ya Masekelo, Abdallah amesema ameamua kujitokeza kutokana na wito wa wananchi pamoja na dhamira yake ya dhati ya kuwatumikia wakazi wa kata hiyo kwa uadilifu, ushirikiano na ufanisi.

Kwa sasa, mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaendelea kwa ajili ya kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya Udiwani kwenye Kata ya Masekelo, pamoja na kata nyingine nchini.












 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA


Post a Comment

Previous Post Next Post