Mwandishi wetu
Ulikuwa ni jumamosi yenye furaha na shangwe kwa Shule ya Awali na Msingi ya Santa Edwin baada ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwana Hassan Mussa Ibrahimu kufunga ndoa na Bi. Bahati Hassan Makala.
Mkurugenzi wa shule hiyo na Mwenyekiti wa Kamati ya harusi hiyo Bwana Edwin Soko amesema kuwa, hatua hiyo ya Mwalimu Mkuu Hassan kufunga ndoa ni hatua ya kupongezwa Kwa kuwa sasa inatoa kibali Cha Mungu Kwa Hassan kuishi katika ndoa halali yenye baraka za Mungu.
Sherehe ya Harusi hiyo ilishuhudiwa na watu mbalimbali wakiwemo, walimu wa Santa Edwin, wazazi, wafanyakazi, majirani na marafiki wa shule, ambao wote walijumuika kwenye ukumbi wa Stress Free Beach unaomilikiwa na Jeshi la Magareza Mkoa wa Mwanza.
Shule ya awali na Msingi ya Santa Edwin inamtakia Kila la heri Mwalimu Hassan kwenye maisha yake mapya ya kifamilia.
Post a Comment