" KATIBU WA CCM MKOA WA GEITA ATOA RAI YA HAKI KWA WAGOMBEA UWT

KATIBU WA CCM MKOA WA GEITA ATOA RAI YA HAKI KWA WAGOMBEA UWT


 Na Mwandishi wetu, Misalaba Media

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita, Alexandarina Katabi, ametoa wito kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Geita kuhakikisha wanatenda haki kwa wagombea wote.

Akizungumza leo, Julai 20, katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Nyankumbu ambako mkutano huo umefanyika, Katabi amesema kila mgombea anayo haki ya kuchaguliwa bila upendeleo wowote.

Amehimiza wajumbe kuhakikisha mchakato wa kura za maoni unaendeshwa kwa uwazi na usawa ili kila mgombea apate kile anachostahili kulingana na juhudi zake.

“Wagombea wote wana haki, kila mtu atavuna alichopanda,” amesema Katabi huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili ya chama na kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mshiriki wa uchaguzi huo.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post