Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Chama cha waganga wa tiba asili TAMESOT kimetoa wito kwa waratibu wa serikali kitengo cha afya kikiwaomba ushirikiano wakuwafikia waganga wa tiba asili katika kutoa elimu ya uhamasishaji juu ya ushiriki wa wiki ya tiba asili ya mwafrika.
Ameyasema hayo Katibu mkuu wa chama hicho Lukas Joseph Mlipu akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Geita kwa lengo la kukutana na waganga wa tiba asili ambapo amesema chama hicho kimeanza ziara yakuwa fikia wanga maeneo mbalimbali ili kuwaeleza umuhimu wa kushiriki maadhimisho hayo ambayo yametambuliwa na serikali.
"Tunaipongeza serikali yetu tukufu kuiweka siku hii maalumu kwa waganga wa tiba asili wa Mwafrika, kwani siku hii inatambua tiba asili ya mwafrika na kuifanya kufahamika kwa Dunia nzima kuwa zipo dawa za asili zinasaidia katika kutibu magonjwa mbali mbali yakiwemo magonjwa ya kuambukizwa na yasiyo ya kuambukizwa pamoja na magonjwa ya mlipuko,
siku hii inaheshimisha Taaluma hii na nchi yetu katika Eneo zima la ulimwengu" amesema katibu mkuu Lukas Mlipu.
Hata hivyo ameeleza kusikitishwa na baadhi ya waratibu wa halmashauri kutoka kitengo cha afya wanaojaribu kukwamisha viongozi wa TAMESOT kwa baadhi ya wilaya akama ambavyo ametolea mfano wa halmshauri ya wilaya Misungwi mkoa Mwanza baada ya kupokea taarifa kutoka kwa viongozi wa chama wakilalamika kukwamishwa katika zoezi la utoaji barua za utambulisho juu ya kuwahamasisha waganga kushiriki ziara ya Katibu mkuu huyo Lukas Mplipu.
"Tunomba ushirikiano kwa waratibu wa tiba asili na tiba mbadala wa Halmashauri zote nchini Tanzania bara baadhi yao wamekuwa kikwazo kwa vyama tunahitaji kusonga mbele bila ya vikwazo." ameendelea kusisitiza katibu mkuu Lukas.
Amefafanua kwamba tayari serikali imewatambulisha wajumbe 15 kwa mwaka huu wakiwemo na viongozi wa vyama vya tiba asili na tiba mbadala watakaoshiriki kikamilifu katika hamasa ya ushiriki wa wiki ya tiba asili ya mwafrika itakayo fanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 25 hadi 31/ 08/ 2025:
Ziara ya Katibu Mkuu inalenga uhamasishaji waganga mikoa 15 ukiwemo mkoa Kagera akiwa ameanzia mkoa wa Geita tangu Tarehe
14/07/2025.
Katika uhamasishaji ameishakamilisha mikutano yake wilaya ya Bukombe na Leo yupo wilaya ya Chato, na tarehe 19/08/2025 atakuwa wilaya ya Geita mjini na kuhitimisha ziara yake wilaya ya Nyangh'wale Mkoani Geita.
Aidha ziara yake itaendelea Mkoani Mwanza Tarehe 21hadi 22/08/2025 wilaya ya Ilemela kata ya Igombe B Kabla ya katibu Mkuu huyo kuelekea Mkoa wa Mara kwa ziara ya siku 2 ambapo tarehe 26 -28/08/2025 atakuwa Mkoani Kagera , Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
Ametoa wito kwa waganga wasisite kushiriki maadhimisho hayo yenye fursa mbalimbali kwao.
Post a Comment