Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imepanga kuendesha zoezi maalum la uchanjaji wa kuku kwa ajili ya kudhibiti milipuko ya magonjwa hatari yanayoshambulia kuku, ikiwemo Kideri (Mdondo), Mafua ya Kuku na Ndui.
Kwa mujibu wa tangazo rasmi kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mwl. Alexius Kagunze, zoezi hilo litaanza tarehe 07 hadi 21 Julai, 2025 na litatekelezwa katika kata, mitaa na vijiji vyote vya manispaa.
Wananchi wote wanaofuga kuku wanahimizwa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo muhimu kwa ustawi wa mifugo yao na uchumi wao. Aidha, chanjo hii ni ya ruzuku kutoka Serikali hivyo itatolewa bila malipo yoyote.
Uongozi wa Manispaa unasisitiza ushirikiano kutoka kwa viongozi wa mitaa na wafugaji ili kufanikisha lengo la kudhibiti magonjwa ya mifugo na kuboresha afya ya kuku katika eneo lote la Manispaa ya Shinyanga.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment