" BODI YA PAMBA YAHAMASISHA KILIMO CHA PAMBA

BODI YA PAMBA YAHAMASISHA KILIMO CHA PAMBA

Na Mwandishi wetu, Misalaba Media BODI ya Pamba Tanzania (TCB) imesema inayatumia Maonesho ya Nanenane Mwaka huu kuhamasisha matumizi ya teknolojia itakayowezesha kuleta mapinduzi makubwa ya Kilimo cha Pamba hapa nchini ili mkulima apate tija ya Kilimo hicho.Hayo yamebainishwa  kwenye Maonesho ya Nanenane  jijini Mwanza na Afisa Kilimo wa TCB, Sharifa Salumu akisema katika maeneo yote ambapo maonesho yanafanyika akitaja mengine Kuwa Nyakabindi Mkoani Simiyu, Ipuli Tabora na  Nzuguni Dodoma Kuwa Elimu ya matumizi ya teknolojia cha Kilimo bora inafanyika.Alisema mkulima anafundishwa mbinu bora za upandaji, unyunyiziaji wa viuwatilifu na mbolea, uvunaji na uuizaji kwa kutumia mizani janja  unahimizwa katika maeneo yote ambapo Maonesho yanafanyika hapa nchini.Salumu alisema kuwepo kwa matumizi ya mbolea hai, matumizi ndege nyuki (drone) na trekta kwa ajili ya kunyunyizia kunamatokeo chanya kwenye KilimoCha Pamba hivyo wakulima katika maeneo yote wanahimizwa kufuata masharti ya teknolojia hizo za kisasa ili wapate hadi kilo 1500 katika ekari Moja.Aliwataka wakulima wa Pamba hapa nchini kushawishika kujifunza ukulima wenye tija kwani manufaa yake ni makubwa yanayomwezesha kupata mazak mengi na hivyo kufurahia Hali hiyo.“Bodi ya Pamba imeweza kununua trekta 400 na kusambazwa katika maeneo yanayolima zao hilo na kuwezesha mkulima Kilimo hicho kulimiwa kwa shilingi 35,000 kwa ekari Moja badala ya 65,000 “ alisema Salumu.Salumu alisema katika Maeneo yote yanapofanyika Maonesho hayo mwitikio ni Mkubwa kwa wakulima Kufika kujifunza Kilimo cha matumizi ya teknolojia yenye tija ili kuboresha Kilimo Chao.Mkulima wa zao aliyefika kupata Elimu hiyo Msafiri Philipo kutoka wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma alisema anafurahia kuwepo kwa mizani janja kwani inawawezesha kuuza Pamba kwa uhakika wa kutokupunjwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post