Na Lydia Lugakila, Misalaba Media
Bukoba
Mhandisi wa TANROAD, Johnston Mtasingwa ameibuka mshindi kwa kupata kura 1,408, akiwabwaga wenzake zaidi ya wanne waliokuwa wakishiriki mchakato wa kumpata Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Bukoba Mjini.
Katibu wa Chama cha mapinduzi jimbo la Bukoba mjini, Shabani Mdohe ametangaza kura za maoni ambapo amewataja wengine waliogombea kuwa ni Alex Denis aliyepata kura 804, Almasoud Kalumuna mwenye kura 640, Jamila Hassan mwenye kura 66, na Koku Rutha aliyepata kura 44.
Alisema kuwa wapiga kura waliojiandikisha ni 3,033, waliojitokeza kupiga kura ni 2,978, kura zilizoharibika ni 20 na kura halali ni 2,958.
Post a Comment