Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kahama kimemtangaza Emmanuel Peter Cherehani kuwa anaongoza katika Matokeo ya awali ya Uchaguzi wa Kura za Maoni ndani ya Chama katika Jimbo la Ushetu ambapo hadi sasa bado Matokeo ya jumla haajajulikana kutokana na Kata Tatu kurudiwa Uchaguzi huo Leo tarehe 05/8/2025.
Kata ambazo zinafana Uchaguzi wa Kura za Maoni ni Ubagwe, Mapamba na Bulungwa kufuatia baadhi ya Wanachama kutoa Malalamiko yaliyokifanya Chama kuchukua Uamuzi wa kurudia Uchaguzi huo.
Akitangaza Matokeo hayo ya awali Katibu Mkuu wa CCM Wilaya ya Kahama Andrew Chatwanga amesema Jimbo la Ushetu lilikuwa na Jumla ya Wagombea Wanne, ambapo Emmanuel Cherehani amepata Kura 5656, Valelia Wilson Mwampashe amepata Kura 153, Machibya Mwambilija Dofu amepata kura 171, na Mussa Shilanga Misungwi Kura 452.
Kwa Matokeo hayo Emmanuel Peter Cherehani ameongoza katika Matokeo ya Awali katika Uchaguzi wa Kura za Maoni ndani ya Chama.
Post a Comment