HomeHABARI KYAISHOZI AWEKA MSISITIZO KWA VIPAUMBELE VYA WANANCHI KATIKA UDIWANI 2025 Misalaba Media August 02, 2025 0 Na Lydia Lugakila, Misalaba Mesia -BukobaJeremiah Justinian Kyaishozi, maarufu (Jeremi Kyaishozi), ambaye ni mzaliwa wa kata ya Kitendaguro katika Manispaa ya Bukoba, Mkoa wa Kagera, ametangaza nia yake na kuweka wazi vipaumbele muhimu kwa wananchi, endapo atachaguliwa kuwa diwani katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.Kyaishozi ametoa maelezo hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, huku akitaja kipaumbele cha kwanza kubwa kitakuwa ni maendeleo, ambapo atahakikisha anapambania uboreshaji wa barabara zitakazo pitika kwa majira yote ya mwaka na zenye kiwango cha lami. Ameeleza kuwa maendeleo hayawezi kupatikana ikiwa barabara hazipitiki, hivyo ni lazima zirekebishwe na kuboreshwa ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao muhimu.Aidha, Kyaishozi ameeleza kuwa atahakikisha wananchi wa kata ya Kitendaguro wanapata huduma bora za afya huku akitamani kuona panakuwepo na kituo cha afya, pamoja na kuboresha shule za msingi, kama vile Bugambakamoi na Kitendaguro.Amesisitiza umuhimu wa mazingira mazuri ya ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi ambapo amesema ataweka mbele masuala ya Elimu.Katika kutekeleza mipango yake, Kyaishozi ameongeza kuwa ataweka juhudi kuhakikisha wazazi wanakuwa na hamasa na kuelewa zaidi kuhusu umuhimu wa elimu kwa watoto wao ikiwa ni njia moja ya kuwasaidia watoto kunufaika na maisha bora ya baadaye, huku akijitolea kusaidia wenye uhitaji.Kyaishozi pia ameahidi kutoa ushirikiano wa karibu, kuheshimu ngazi za kimamlaka, pamoja na kuhamasisha umoja na mshikamano ndani ya chama chake cha mapinduzi (CCM) ili kufanikisha mipango mizuri ya maendeleo.“Mimi nikifanikiwa kupata nafasi ya udiwani, udiwani huo utakuwa sio wangu bali wa wananchi, kutokana na maendeleo na kiu niliyonayo ya maendeleo kwao," alisema Kyaishozi. Kyaishozi amewasilisha historia yake ya uongozi, akisema alianza darasa la kwanza katika shule ya msingi Bugambakamoi ambapo akiwa kiongozi wa wanafunzi tangu darasa la kwanza hadi alipomaliza darasa la saba ambapo kuanzia mwaka 1993, amekuwa akihusika katika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya chama na serikali huku akiwa kiongozi wa umoja wa vijana, mjumbe wa mtaa na mweni wa mtaa akiongoza hadi mwaka 2014. Ameeleza kuwa kuwa baada ya hapo, aliendelea kujifunza siasa akiwa nje ya uongozi kwa zaidi ya miaka 10.“Mimi nina nia nzuri ya kuwaongoza wananchi nikiwa diwani kwani sina shaka wananchi wana imani na mimi,” alihitimisha Kyaishozi.KARIBU CHUO CHA MADINI SHINYANGA (EARTH SCIENCES INSTITUTE OF SHINYANGA)🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA You Might Like View all
Post a Comment