" RUZINGA MPYA YA KIMATAIFA TWENDE NA ASPON MUCHUNGUZI MWIJAGE MGOMBEA UDIWANI KATA RUZINGA

RUZINGA MPYA YA KIMATAIFA TWENDE NA ASPON MUCHUNGUZI MWIJAGE MGOMBEA UDIWANI KATA RUZINGA


Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaWananchi katika kata ya  Ruzinga Wilaya Missenyi   Mkoani Kagera wameahidi kutofanya makosa katika kuchagua kiongozi mwenye mabadiliko huku wakiahidi kumchagua Aspon Muchunguzi Mwijage kutokana na mazuri aliyoyafanya ndani ya  kata hiyo kabla ya kugombea nafasi hiyo ya udiwani jambo linalokwenda kufanya Ruzinga kuwa ya kimataifaWakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao akiwemo Evodius Khawa na Helena Jonas wamesema kuwa wao wapo tayari kuendana na kiongozi mwenye kuwajali wananchi na  kuwaletea mabadiliko.Evodius amesema kuwa  Mwijage amekwisha toa mwanga mpya kutokana na namna ambavyo amekuwa akiwagusa wananchi wa kata ya Ruzinga na maeneo jirani hasa  kwa kuijali zaidi jamii inayomzunguka."Tumevutiwa sana na mgombea huyu maana katika kujinadi ameahidi Posho atakayoipata akiwa katika nafasi ya udiwani atahakikisha inahudumia shule tatu ikiwemo shule ya msingi Ruzinga,Mugongo na Ruhija" alisema Mwijage.Wananchi hao wamesema kuwa wana imani na Mwijage baada ya  kiwaahidi kutengeza barabara ya kuunganisha Ruzinga na Buyango kupitia kwenye tinga tinga tatizo  ambalo limewasumbua kwa zaidi ya miaka 20.Aspon Muchunguzi Mwijage ambaye ni mtaalamu wa jiolojia (geologist) mwenye uzoefu mkubwa katika sekta ya utafiti wa madini na mfanyabiashara katika sekta tofauti nagombea kiti cha idiwani alihitimu masomo yake ya jiolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 1992.Anahusika katika miradi ya kijamii, ikiwa ni pamoja na mradi wa Trends Earth unaolenga kufuatilia na kutathmini hali ya uharibifu wa ardhi kwa kutumia teknolojia ya kisasa huku akiwa mwenyekiti na mjumbe wa bodi za tasisi mbalimbali za elimu, dini, na maendeleo ya jamii.mtia nia huyo ameshika nafasi muhimu katika kushirikiana na wana Ruzinga kuleta maendeleo kupitia tamasha la Ruzinga Day  linaloratibiwa na Ruzinga Development (RD) ambapo ametaja dhamira ya  kugombea udiwani wa kata ya Ruzinga kuwa  ni kikabiliana na changamoto na nyufa mbalimbali zilizojiokeza katika kipindi kilichopita ikiwa ni pamoja na kuhakikisha anawauganisha wana Ruzinga katika juhudi za kujiletea maendeleo ikiwemo kuleta amani na utulivu katika jamii ya wana Ruzinga.Ameongeza kuwa endapo akichaguliwa vipaumbele vyake vitakuwa kitatua kero ya uji kwa shule za msingi za Ruhija, Mugongo na Ruzinga,kutatua changamoto ya mlinzi wa zahanati,  kuhakikisha ujenzi wa OPD unakamilika,kuanzisha ujenzi wa ofisi ya kata CCM, Kuvunja kambi zote mbili za kisiasa ili kuwa kitu na kuwa itu kimoja.Aidha amesema atasaidia juhudi za Serikali katika kusambaza umeme, barabara, na maji; kuwalipia watu wa kila kitongoji ambao hawana uwezo wa kujilipia umeme.  "nitaendelea na zoezi la kugawa madaftari katika shule zote za msingi katani Ruzinga ikiwa ni pamoja na kutoa motisha kwa watoto wa darasa la 4 na la 5 kufanya utalii mjini Bukoba ikiwa ni pamoja na kupima mashamba yote ili yaingie katika malipo ya hewa ukaa" alisema Aspon.Ameongeza kuwa hadi sasa wengine tayari wameshayapata malipo sambamba na kutoa ushauri na kutafuta leseni ndogo za uchimbaji wa madini yenye thamani kwa vijana pamoja na kushirikiana na jamii katika kuendesha miradi ambayo itakuwa imeibuliwa.


Post a Comment

Previous Post Next Post