UTANGULIZIEmmanuel Bulunja LUHEMEJA ni miongoni mwa wagombea tisa waliopitishwa na Kamati Kuu ya CCM Taifa, akiwa Mteuliwa Na. 5 kwa Jimbo la Ilemela. Ni kiongozi kijana, msomi, mtaalam na mzalendo ambaye ameonesha kwa vitendo uwezo wake wa kuchochea maendeleo kupitia maarifa, weledi na moyo wa kujitolea. *UZOEFU NA UMAHIRI* LUHEMEJA ni mtaalamu mahiri wa masuala ya fedha na usimamizi wa biashara, akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 13 ndani ya Kanda ya Ziwa. Tangu alipohitimu Shahada yake ya Kwanza mwaka 2011, amejikita katika kuwawezesha wajasiriamali wa viwango vyote wadogo, wa kati (SMEs) na wakubwa kupitia mafunzo ya kiuchumi, elimu ya fedha na uongozi wa biashara.Anasifika kwa kuwa na maono ya maendeleo jumuishi, uwezo wa kufanya maamuzi yenye busara na weledi wa hali ya juu katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi. *SHUGHULI ZA KISIASA NA KIJAMII* Mwanachama hai wa CCM tangu mwaka 2005, LUHEMEJA amekuwa mstari wa mbele katika shughuli za chama, akiwa kiongozi ndani ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa na Mratibu wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2025. Katika nafasi hizi, amejitokeza kuwa daraja muhimu kati ya chama na wananchi, hasa katika kuhamasisha: *Elimu ya fedha* *mashuleni na mitaani* Ujenzi wa uwezo kwa wanawake na vijanaKupambana na utegemezi wa ajira kwa kuimarisha sekta ya ujasiriamali *MAONI YA WANANCHI WA ILEMELA* Sauti za wananchi kutoka kila kona ya Ilemela zinaonyesha imani kubwa kwa LUHEMEJA: “Tunamhitaji mtu wa vitendo kama LUHEMEJA. Ameonesha kuwa maendeleo hayawezi kutegemea siasa pekee, bali mipango thabiti ya kiuchumi.” Mkazi wa Nyasaka" *LUHEMEJA* amekuwa nasi kwenye misiba, harusi, mashindano ya vijana, hadi midahalo ya maendeleo. Huyu ni wa kwetu kweli kweli.”Vijana wa Buswelu"Kwa utaalamu wake wa fedha, tuna hakika ataweza kuleta uwekezaji wa maana na kukuza miradi ya ujasiriamali.”Kijana mjasiriamali wa Pasiansi *TAALUMA NA MAENDELEO BINAFSI* LUHEMEJA ni mfano halisi wa kiongozi msomi anayejifunza bila kuchoka. Ana:Shahada ya Kwanza: Mahusiano ya KimataifaShahada ya Uzamili: Usimamizi wa Rasilimali WatuStashahada ya Juu ya Uzamili: Diplomasia ya UchumiShahada nyingine ya Uzamili: Maendeleo na Ushirikiano wa KimataifaKwa sasa: Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika chuo kikuu hapa nchini.Ujuzi huu unamweka katika nafasi bora ya kuelewa kwa kina sera, diplomasia ya maendeleo na changamoto halisi za wananchi wa kawaida. *DIRA YA UONGOZI WAKE* *Kama Mbunge, LUHEMEJA ana maono ya Ilemela mpya yenye* :Uwezeshaji wa vijana na wanawake kupitia mikopo midogoUshirikiano kati ya sekta binafsi na serikali katika afya, elimu na miundombinuElimu ya fedha katika familia ili kupunguza utegemeziUshiriki wa wananchi katika kupanga vipaumbele vya maendeleo *KAULI YA MGOMBEA MWENYEWE* “Nimeingia kwenye kinyang'anyiro si kwa ajili ya heshima binafsi, bali kwa mapenzi yangu makubwa kwa Kiongozi wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameonyesha njia ya kweli ya maendeleo kwa vitendo. Ilani ya CCM 2025-2030 imejaa majawabu ya changamoto za Ilemela, na mimi niko tayari kuisimamia kikamilifu kwa niaba ya wananchi.” *HITIMISHO* Tarehe 04 Agosti 2025, simama pamoja na kizazi kipya cha viongozi wa vitendo. Mchague kwa kura ya NDIYOMtetezi wa wananchi, mzalendo wa kweli, kijana wa maendeleo."Kwa msingi wa uadilifu, uaminifu na utendaji uliothibitishwa, LUHEMEJA ndiye chaguo la Ilemela Mpya.” *CCM OYEEEEE!* *LUHEMEJA OYEEEEE!* *Ilemela Mpya, na LUHEMEJA Inawezekana!*

Post a Comment