" MHANDISI JOHNSON JOHANSEN MUTASINGWA AHADI KUIBADILI BUKOBA MJINI KWA MAENDELEO

MHANDISI JOHNSON JOHANSEN MUTASINGWA AHADI KUIBADILI BUKOBA MJINI KWA MAENDELEO

Na Lydia LugakilaBukobaMgombea wa ubunge Jimbo la Bukoba mjini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi Johnson Johansen Mutasingwa, ameahidi kuibadili Bukoba mjini  endapo wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi watashirikiana kwa pamoja katika kuondoa makundi ndani ya chama hicho.Mutasingwa ametoa kauli hiyo Agosti 25,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Manispaa ya Bukoba, muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo. Amesema ushindi alioupata wa kugombea nafasi hiyo sio wa kwake pekee bali ni wa chama cha Mapinduzi, hivyo ni wakati sasa kwa wanachama hao kushikamana na kushirikiana ili kuliletea maendeleo Jimbo hilo."Nawaomba tushikamane, tuepuke makundi na tuyavunje ili tuwe kitu kimoja aliyeshinda sio mimi mhandisi, bali huu ni ushindi wa CCM hivyo tupambane tupate kura nyingi za wabunge, madiwani na Rais, kwani hakuna asiyejua mengi na makubwa aliyoyafanya Rais wetu mpendwa," alisema Mutasingwa.Mhandisi huyo amewashukuru wananchi waliomsindikiza kuchukua fomu hiyo huku pia akikishukuru chama chake upande wa wilaya na taifa kwa kuliona jina lake kuwa linafaa na kurudi.Ameahidi kuwafanyia makubwa wananchi wa Jimbo la Bukoba mjini na kuongeza kuwa  maendeleo hayana chama, hivyo atawatumikia wananchi wote kwa hekima na utiifu mkubwa, huku akisisitiza kuwa umoja ndio nguzo ya kukipa ushindi chama hicho, wala si kutengana na kuneneana mabaya.Kwa upande wake, msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini, Melkion Komba, ametoa maelekezo kwa mgombea ubunge huyo na kusema tayari barua anayo na imekidhi misingi yote, hivyo kazi imebaki kwake kujaza fomu hizo kwa utaratibu uliopo ili kuirejesha kwa muda husika, ambapo mwisho ni Agosti 27, 2025.

GUSA LINK HAPA CHINI👇


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post