Na Neema Sawaka, KahamaMkurugenzi wa taasisi za Rocken Hill na Anderlek Ridges iliyopo Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga Alexander Kazimil amewashauri wazazi kutochoka katika kufundisha matumizi mazuri ya teknolojia yanayoendelea kuwepo na kuepukana na Matumizi ya madawa ya kulevya kwa vijana.Kazimil amesema hayo katika Mahafali ya 21 ya darasa la saba na Mahafali ya 17 ya kidato cha nne huku akieleza mtoto akimaliza kidato cha nne sio kumuachaniza kwa madai amekuwa bila kumkumbushia maadili na malezi mema na nidhamu katika jamii.Kazimil amesema tecknolojia ni nzuri nani mbaya haiwezi kukwepeka kwa watoto hivyo jitihada zinahitajika kwa wazazi,walimu na jamii nzima kuhakikisha watoto wanapata malezi na kuwakumbusha kila siku kutotumia madawa ya kulevya."Muwaeleze watoto kuwa wavumilivu kwani maisha yanaweza kuwa juu au chini nakutambua vipaji walivyonavyo ambavyo vitawasaidia kujipatia ajira na kuendeleza maisha yao"amesema Kazimil.Kazimil amesema vijana wanatakiwa kuandaliwa kiimani na kimaadili kwani wapo wazazi wengine wamekuwa wakilea watoto wao kama mabosi kwa kuogopa hata kuwatuma kazi majumbani kwani wakifanya hivyo wataweza kutengeneza kizazi kisicho bora hapo baadaye.Kazimil amesema elimu siyo ya kuchezea na kwani ndiyo inayoendesha maisha haimuondolei mtu umasikini bali inamtaka kila mmoja kujifunza na kupambana na wimbi la umasikini na watu wasiwakatishe tamaa.Mkurugenzi wa Shule za msingi Rocken Hill Dkt Zephania Madaha amesema shule hizo zinawahitimu 186 wa darass la saba zimekuwa zikifundisha masuala ya Mshikamano,maadili na imani kwani wameona dunia inavyokwenda na kuwataka wawe na hofu ya mungu ili waweze kutimiza ndoto zao.Naye Mkurugenzi wa shule ya Anderlek Ridges Godwin Ng'osha amesema wamekuwa wakifanya viziri kitaaluma nakuwapongeza wazazi kwa kuwaamini kuwa na watoto wao muda wote kwa kipindi cha miaka minneMgeni rasmi katika mahafali hayo katibu wa baraza la ushauri la wazee. Anderson Lyimo amesema watoto wasipolelewa vizuri watamomonyoka kimaadili nakuwa taifa la watu wa hovyo hivyo mafundisho mema yaendelee ndani ya familia ili nchi iwe ya amani na utulivu hasa kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.mwisho.

Post a Comment