MSIMAMIZI WA UCHAGUZI WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI, MWL. ALLY
LIUYE (kushoto) AKIMKABIDHI FOMU ZA UTEUZI WA MGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA
SHINYANGA MJINI NDG. ABDALLAH SUBE (kulia)
Na Elias Gamaya- Shinyanga
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mwl. Ally Liuye leo Oktoba 14, 2025 amekabidhi fomu za uteuzi kwa mgombea wa nafasi ya Ubunge Ndg. Abdallah Sube kwa jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia chama cha AFRICAN DENOCRATIC ALLIANCE (ADA- TADEA).
Ndg. Sube anakuwa mgombea wa Kwanza kuchukua fomu za Uteuzi wa wagombea ubunge kwa jimbo la Shinyanga Mjini ambapo ambapo jumla ya vyama 11 vilivyosajiliwa kwa jimbo hili vinatarajiwa kushiriki katika mchakato huo.
Zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi ya Ubunge umeanza rasmi leo Agosti 14, 2025 ambapo unatarajiwa kutamatika Agosti 27, 2025 ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Post a Comment