
Vyama vya siasa nchini vinaendelea kunadi sera zake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, ambapo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kwimba, mkoani Mwanza, Cosmas Bulala, amezindua rasmi kampeni zake katika Kata ya Hungumalwa.
Katika uzinduzi huo, Bulala amewataka wananchi wa jimbo hilo kumpa kura nyingi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na kumpa yeye kura ya ubunge na kuwachagua madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili waweze kushirikiana katika kuwatumikia wananchi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment