" MSAADA WA KISHERIA KUTOLEWA KATIKA MAGEREZA 18 KANDA YA ZIWA

MSAADA WA KISHERIA KUTOLEWA KATIKA MAGEREZA 18 KANDA YA ZIWA







Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza Tanzania inatarajia kutoa Huduma za Msaada wa Kisheria katika Magereza 18 yaliyoko Kanda ya Ziwa katika mikoa ya Mara, Mwanza, Simiyu na Shinyanga.

Akizungumza Mjini Morogoro wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam watakaotoa Huduma za Msaada wa Kisheria katika Magereza hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Ester Msambazi amesema kuwa huduma ya Msaada wa Kisheria inatolewa Magerezani na maeneo ya Vizuizini ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Msaada wa Kisheria ya mwaka 2017 iliyofanyiwa maboresho 2023.

“Sheria hii inatuelekeza kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi wasio na uwezo na wale walio vizuizini, tumetekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia nchi nzima lakini hatukuweza kuwafikia mahabusu na wafungwa, hivyo tumeona ni vyema kuwafikia na kuwapa huduma za Msaada wa Kisheria kama sheria inavyoelekeza” amesema Msambazi.

Naye Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Haruna Matata amesema lengo kubwa ni kutoa msaada wa kisheria katika maeneo ya Vizuizini na Magerezani ni kupunguza msongamano katika maeneo hayo, pamoja na kutekeleza takwa la kikatiba na kisheria linaloagiza mtu yeyote asiyekuwa na uwezo kupewa Msaada wa Kisheria.

Ameeleza kuwa utekelezaji wa zoezi hilo utaanza tarehe 22 Septemba, 2025 ambapo huduma mbalimbali za kisheria zitatolewa ikiwemo elimu, uandaaji wa nyaraka za kisheria kama vile nyaraka za rufaa, kuwasaidia mahabusu kufahamu mienendo ya mashauri yao pamoja na msaada wa uwakilishi mahakamani.

Kwa upande wake SSP Demetrius Masala, Mratibu wa Huduma za Msaada wa Kisheria kutoka Jeshi la Magareza, amesema kuwa utoaji Msaada wa Kisheria katika Magereza utawasaidia mahabusu waliokosa haki kupata haki zao katika kipindi cha muda mfupi, aliongeza “Katika Magereza zetu, watu wengi walioko huku hawajui kusoma na kuandika, hivyo kwa Elimu na Msaada wa Kisheria unaoenda kutolewa wengi watasaidika, wanaohitaji kuandaliwa maombi ya dhamana, rufaa na nyaraka mbalimbali watapata pia”.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA


Post a Comment

Previous Post Next Post