Na Lydia Lugakila, Misalaba Media
Mkuu wa wilaya ya Kyera Mkoani Kagera Zaitun Msofe ametangaza ujio wa Mwenge wa uhuru
unaotarajiwa kupokelewa wilayani Kyerwa mnamo Septemba 11,2025 katika eneo la Mabira ambapo katika eneo hilo kutakuwa na miradi miwili itakayozinduliwa ikiwemo mradi wa Barabara ya lami na mradi wa maji.
Msofe amesema Mwenge huo utafika katika kata ya Kitwe ambapo kutakuwa na mradi wa kitalu cha miche na baada ya hapo utapita Kamuli na baadaye Nyakatuntu ambapo katika eneo hilo kutakuwa na banda la Elimu ya uchaguzi ili kuwawezesha wananchi kupata elimu ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.
Mwenge huo wa uhuru ukiwa Nyakatuntu utatoa ujumbe wa Mwenge pia kutakuwa na zoezi la usafi wa mazingira.
Amesema kuwa baada ya Nyakatuntu Mwenge huo utafika katika kata ya Kyerwa ambapo huko kutakuwa na miradi takribani mitatu ambapo utazindua Benki ya CRDB kwa maendeleo ya wananchi wa Kyerwa pia mradi wa vijana na mradi wa uwanja vya michezo.
Dc Msofe ameongeza kuwa Mwenge huo wa uhuru pia utakwenda Rukuraijo ambapo huko kuna mradi wodi ya wazazi katika zahanati ya Rukuraijo ambapo baada ya hapo utakwenda Muhulire shule ya msingi kutakuwa na mradi wa madarasa,na Ofisi baada ya hapo Mwenge huo wa uhuru utapelekwa stendi ya Nkwenda kwa ajili ya mkesha.
Amewaomba wananchi wilayani humo kujitokeza kwa wingi kuupokea na kuushangilia mwange huo wa uhuru.
Hata hivyo amewakaribisha wananchi wote, viongozi wote wa Taasisi na binafsi wafanyabiashara, wakulima kujitokeza ili kukesha na Mwenge wa uhuru ambao umebeba ujumbe usemao jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment